Toyota Camry 9th Generation (2025): Aisee Designer wa Toyota Aongezewe Mshahara!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Wakuu.

Kuna hii generation ya tisa ya Toyota Camry mpya, model code XV80, itakayoingia mzigoni mwakani (2025) aisee ina kila sifa za kua gari kali, kuanzia muonekano ndani na nje hadi performance yake.


Kwa muonekano wa nje, inakuja kwa shape ya sedan tu, na mbele imechukua new generation ya Prius na Crown, ila chasis imebaki ya generation ya nyuma.



Nyuma kuna LED tail lights zilizoingia hadi kwenye buti, na chini exhaust pipe zimefichwa kwa chini.

Kwa ndani chuma ipo classy sana. Kuna screen kubwa yenye Apple CarPlay na Android Auto, pia ina instrument cluster moja ya LCD tamu sana.




Kwa upande wa engine, Kuna option ya hybrid au pure gasoline, zikija na engine ya 2.0L au 2.5L!


Tuendelee kusubiria ziwe used, by 2030 tutamiliki vyuma vikali sana wanangu.
 
Tuendelee kusubiria ziwe used, by 2030 tutamiliki vyuma vikali sana wanangu.
🤣🤣🤣 Daah ila wenzetu wanatumia gari muda mfupi aisee yaani itoke 2025 then 2030 wazee wa used tuipate.

Na sisi tukiipata hiyo 2030 ni mpaka ipate ajali mbaya mbaya mno, isiyotamanika ndio itauzwa kama vyuma chakavu na hiyo ni by late 2040's.
 
naona tu ni trend ya mwonekano wa kitesla, tesla model 3 sawa na ilivyo kwa BYD
 
Kama mashoga na wauza miili wanavyobadili I phones Tanzania.
 
Nje ya mada kidogo, hivi serikali inashindwa nini kuanzisha kiwanda cha magari bongo tupate vyuma kama hivi 0km

TRA wachukue kodi yao kwenye mchakato mzima wa upatikanaji wa Gari kuanzia kuchimba chuma, kufanya refinery ya chuma, kuunda magari na kuuza magari kote huko wachukue kodi naona kama itakua sawa tu na hii kodi ya magari ya mtumba.

Naona kama uwezo tunao ila tunalazimisha kua dampo la vyuma chakavu kutoka Asia na Europe
 
kutengeneza magari sio sawa na kutengeneza nazi za azam mkuu inahusisha mambo mengi na ndio maana utakuta ni brand zile zile tu zimefungua viwanda nchi nyingine.
Wewe uko tayari kununua brand ya kitanzania ambayo inatengeneza gari ambalo lina tech ya mgongo wa chura ya mwaka 1930 wakati kuna gari ya mjapan ya mwaka 2002 ina technolojia nzuri used?
Labda ishawishi brand za magari kubwa kama toyota au vw ijenge kiwanda hapa na usitegemee gari zitakuwa cheap. tafuta hata passo toleo la miaka hii mitatu au minne tazama bei yake utashangaa hapo hujalileta hapa. ndio maana tunaishia kununua gari zilizopitwa na wakati.
 
Combustion engine zitaendelea isipokuwa nishati ndio itabadilika kwa kutumia hydrogen badala ya petrol, ndio maana Toyota hakimbilii BEV isipokuwa amejikita kwenye kutafuta fuel isiyochafua mazingira na kutolazimika kubadili production line. Kwa sasa anaboresha ufanisi wa gari ya kutumia maji kuzalisha hydrogen kwa electrolysis ambayo baada ya combustion inatoa tena maji badala ya carbon, niliiona YouTube wanaielezea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…