Toyota game changer full EV Vehicle

Extrovert

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2016
Posts
70,785
Reaction score
186,690
Baada ya mtanange wa kuelekea katika ukurasa mpya wa teknolojia endeshi ya Magari ukiongozwa na mshika mwenge "Tesla Motors" hatimae mwaka 2020 ulikuwa mwaka wa mapinduzi sana ambapo asilimia 80 ya makampuni ya waundaji magari walileta walau toleo moja la full electric vehicle yani gari ambazo zinaendeshwa kwa battery za kuchajiwa mithili ya tunavyochaji simu.

Hatimae mwaka 2021, Kampuni yetu pendwa Toyota wakishirikiana na Subaru nao wametuletea kitu kipya ikiwa ni advancement ya teknolojia ya gari ambayo nayo ni full EV. Tofauti na wengine wao watatumia static battery tech ambayo itawezesha gari kuchajiwa kwa dakika 10 tu. Hii gari itakuwa ni mapinduzi makubwa kwa wale vijana wenzangu wenye allergy ya kwenda sheli maana itakuwa ni ya kuchaji tu kama simu. Kwa muundo pia ina shape nzuri ya kuvutia sana na iko na ukumbi wa kutosha sana ndani.

 
Hawa wehu bila kuandamana wataleta mazoea 😂😂😂!!! Inabidi tukaze nyoro tupaze sauti gari za umeme zisilipiwe kodi ili ku encourage watu wengi wazinunue.
Kuandamana hakusaidii kitu. Wao akili ni kupata mapato tu. Yaani watatoza kodi hata mara kumi zaidi. Labda upange mapinduzi ya kijeshi na mabrigedia halafu wewe ujitangaze Rais kwenye TBC, halafu wewe ndie urekebishe kodi.
 
mchina ana EV anaiuza shilingi za kitanzania milioni 10 mpyaaaa, na nasikia inauza zaidi ya Tesla sasa hivi. Gari inaitwa Hong Guang Mini EV, dola 4500 tu mpyaaa unaimenya kwenye maganda.
 
My heart dwells in Germany, Bavaria Motor Works
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…