Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 70,785
- 186,690
Baada ya mtanange wa kuelekea katika ukurasa mpya wa teknolojia endeshi ya Magari ukiongozwa na mshika mwenge "Tesla Motors" hatimae mwaka 2020 ulikuwa mwaka wa mapinduzi sana ambapo asilimia 80 ya makampuni ya waundaji magari walileta walau toleo moja la full electric vehicle yani gari ambazo zinaendeshwa kwa battery za kuchajiwa mithili ya tunavyochaji simu.
Hatimae mwaka 2021, Kampuni yetu pendwa Toyota wakishirikiana na Subaru nao wametuletea kitu kipya ikiwa ni advancement ya teknolojia ya gari ambayo nayo ni full EV. Tofauti na wengine wao watatumia static battery tech ambayo itawezesha gari kuchajiwa kwa dakika 10 tu. Hii gari itakuwa ni mapinduzi makubwa kwa wale vijana wenzangu wenye allergy ya kwenda sheli maana itakuwa ni ya kuchaji tu kama simu. Kwa muundo pia ina shape nzuri ya kuvutia sana na iko na ukumbi wa kutosha sana ndani.