Toyota Hillax Pick up, 2012

Kwema dagii unataka bmw X 3 ya mwaka gani zipo za diesel na petrol ipi unahitaji ingawaje bima za diesel maintanance katika spare ni ghari zaidi ya za petrol...
 
Kruger hiyo picha ni pick up ya 2016 na 2017 V 8 hizo nakujulisha bei ya 2010 mpaka 2015 nyingi ni v6 kurekebisha ya ajali ni nafuu SA kuriko Arusha unampa dealer tuu mwezi ipo kama mpya inategemeana na ajali yake...ila kama unataka ya 2017 ya ajali pia zipo ila kwa bongo hata ukipata ya 2010 bado ni toleo la karibuni kodi na bei yake itakua chini kidogo...
 
Safi sana mkuu Isanga family kwa ufafanuzi, so ya 2010 iliyopata ajali wakirekebisha, I mean kununua, kutengeneza, kuisafirisha na kodi ya hapa bongo inaweza ni gharimu sh ngapi? Mkuu
 
Ok chukua iliyogongwa headlight kidogo au bumper hizo unazikuta kuanzia tsh 18milion mpaka tsh 23milion unabadilisha taa au bumper unamwaga oil,plug na filter na kupata police clearance ya interpol na safari inaanza ni d4d 3liter diesel johanesburg mpaka tunduma 2800 km hesabu ya mafuta piga hapo...karatasi za interpol bure ni service tuu na kulipia entry boarder mbili zimbabwe na zambia kama usd 150 kila boarder na tollfees za barabara 40usd...kodi Tanzania ni 20milion wastani wa tsh 40m mpaka 45milion inategemeana na bei uliyonunua na jinsi ulivyozunguka kupata gari ya bei cheee maana scrap yard na minada ni mingi sana...
 
Dagii ok hiyo bima 3 ya kuanzia 2006 mpaka mpaka 2008 zinaanzia tsh 12milion mpaka 17m bei zake hazipungui kwa kuwa sokoni hivyo vigari vinapendwa sana model za sasa hivi ndio zipo juu sana pamoja kwamba model hizo zinakua zipo katika hali nzuri ila kodi sijajua ipoje gari ambazo johannesburg ni deal pia mimi huwa sihangaiki nazo mnadani kunakua na ushindani sana tofauti na zingine...
 
Nakushukuru sana Ndugu yangu hadi hapo umenipa mwanga mkubwa sana kuhusu hili, barikiwa sana
 
Mkuu Isanga family, hv nikinunua gari hapo south ikiwa na registration number za huko nikaja nayo hapa nchini, kabla ya kubadili namba naweza tumia hata kwa miezi sita ndipo nibadili? Na je kabla sijabadili siwezi kulipia kodi si ndiyo au kodi haijalishi kama ina namba za south au la?
 
Kruger sheria ya Raia wa Tanzania kuingia na gari ya reg za nje na kutumia inatakiwa uwe na permanent resident ya nchi uliyonunua gari na kusajiliwa na uwe unaishi huko ushakua nje ya Tanzania zaidi ya miezi sita nadhani ila kwa kuondoa usumbufu tafuta na kodi yao ulipe uingie maana gari akiendesha mtu mwingine zaidi ya mwenye vibali inakamatwa na TRA unaweza kwenda ukanunua gari mbili tofauti moja unauza Tunduma inalipa kodi kirahisi au ukabeba bidhaa ambazo zikifika zinauzwa zinalipa kodi ya gari yako...
 
Daa kama vipi kamata ford ziko powa sna aisee.ford puck up naona mm ni imala zaidi ya hizo hilux
 
Nakushukuru sana Ndugu yangu hadi hapo umenipa mwanga mkubwa sana kuhusu hili, barikiwa sana
Mkuu unaweza kunipa mwanga Volkswagen Amarok pick up naweza kupata kwa bei gani? Nitashukuru

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app
 
Savius Cruiser nyingi zipo mpumalanga mashambani mjini zilizopo ni zilizopata ajali huko kwa mwaka huu sijakwenda mwezi wa nane ntakua huko tukijaaliwa ntakupa bei ya shamba..unataka pick up au
mkuu hukunipa mrejesho nahitaji pick up
 
mkuu hukunipa mrejesho nahitaji pick up
Mkuu hujasema unataka pick up aina gani? Toyota d4d,Ford Ranger, Nissan au kwa ununuzi hazina bei kodi Tanzania ndio imesimama kutokana na Mwaka na aina ya pick up...na pia naweza kukushauri ukiweza agiza UK pick up zipo bei chini kuliko SA na Japan na nzuri pia...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…