Toyota hizi...!

Hii ni frame ya Audi A8.. Unaweza kuona ilivyoimarishwa sehemu muhimu za usalama
 
Toyota crown new model body n chassis... See the in it
Gari nyingi za kiJep hazina chassis frame bali body imeungwa direct na chassis fulani very simple... Hii ukipata nayo ajali.... Ni majaliwa ya mola kutoka mzima
 
pole kwa wafiwa
changamoto nyingi za ajali zinachangiwa na sababu zifuatazo
  • wengi tunajua kuendesha gari lakini hatujui matumizi ya barabara
  • hatutambui kuwa udereva ni taaluma ya mtu na hivyo tunahitaji kuieshimu na hasa tunapokwenda safari ndefu ni bora kukodi dereva akusaidie kisha mpe nauli na posho kidogo arudi kuliko kuhatarisha kifo na mali yako.
  • hatuzingatii service kwa ajili ya safari ikiwa ni pamoja na kuangalia muda uimara wa mataili inawezekana kabisa taili zimekwisha muda wake lakini wewe unakanyaga
  • hatuangalii muda mwingi mabadiliko ya gari tukiwa safarini
  • hatujipi muda wa kupumzika tukiwa njiani pamoja kuwa sio wazoefu matokeo yake tunasinzia
  • hatujui umuhimu wa kuwahi ni pamoja na kuanza safari mapema kwa mwendo wa kawaida ila tunaamini kuwahi ni kukimbia
  • mpangilio mbaya wa chakula na vinywaji tukiwa tunaendesha.
yapo mengi ila mengine yatajaziwa na wengine labda mapendekezo kwa uchache
  • hakikisha usisafiri peke yako ikiwezekana chukua hata abiria mmoja anaweza kukuweka bize na kukuepusha na ajali njiani kwa kukupunguzia usingizi japo (kwa angalizo) si salama pia kuchukua abiria mwanamke mzuri mmoja peke yake uko naye mbele kama abiria unaweza ukakuta anakuegemea na kukushikashika ili asilipe nauli mwisho wa siku akakufungua zipu nauli asilipe na ukizidiwa unaweza kusababisha ajali likitokea hili sina uelewa kama unauwezo wa kukemea hivyo kwa usalama park gari mshushe kisha uendelee na safari.
  • jifunze kusimama na kununua zawadi kwa safari unayofanya hii itakupa mapumziko kwa namna fulani na ifuatayo inaweza kuwa mapendekezo kwa safari ya dar-dodoma
    • endesha gari mpaka njia panda ya Mpwapwa simama na shuka chukua nyama ya kuchoma ikisaidie kutafuna isilete usingizi ukiwa njiani kwa kuwa inawezekana ulitoka umekunywa mtori dodoma (japo mtori sio mzuri kwa uendeshaji huwa unaleta usingizi)
    • ukifika gairo au kwa mbele kidogo unaweza chukua maharage na chakula kwa ajili ya nyumbani
    • njia panda ya tuliani chukua mhindi wa kuchoma na wachukulie watoto mahindi watachemsha ukifika
    • ukifika Morogoro kula chakula cha mchana na ikiwezekana pumzika kwa dakika 15
    • vuta mpaka chalinze acha ubahiri chukua korosho za buku 2 na wenzio wametumwa pesa nyumbani unaweza kuchukua pia kwa ajili ya watoto japo kwako pia ni muhimu kama wewe ni mwanaume zikusaidie kuaactivate safer iliyokuwa chini kwa kazi nyingi dodoma usije ukaunder perform halafu usieleweke. kwa safari zitakusaidia kuondoa usingizi kwa kuwa wakati mwingine foleni huanzia Ruvu ukajikuta unakanyaga mafuta badala ya break.
    • Ukifika Ruvu darajani shuka kwa ajiri ya aja ndogo na kunyoosha viungo na kwa kuwa muda huu utakuwa umebakisha km zisizozidi 80 utafika salama.
 
Picha inamuonyesha marehemu kabla ya ajali,na baada ya ajali...swali MPIGA picha kabla ya ajali nani? maana hii picha inaonyesha imepigiwa kati kati ya safari na marehemu hakuwa peke ake kuna mtu alikua nae na ndie alie mpiga picha,swali ni picha nani kazipiga Hasa hyo ya kwanza marehemu akiwa hai.
 
Kukimbiza gari kuna utamu wake..ukiendesha chombo cha mafuta macho muda wote yacheze kwenye Dashboard la sivyo unaeza jikuta upo speed 170 ukahisi kama gari ipo 40..ukifunga Viooo huwezi hisi kabisa mwendo wa gari.
 
Kimbia speed zaidi ya 150kph kwasababu tu inabidi ukimbie,lakini sio kwasababu speedometer inasoma 180 kph basi wewe huo unaufanya ndio mwendo wako hata pasipo stahili....
 
Kukimbiza gari kuna utamu wake..ukiendesha chombo cha mafuta macho muda wote yacheze kwenye Dashboard la sivyo unaeza jikuta upo speed 170 ukahisi kama gari ipo 40..ukifunga Viooo huwezi hisi kabisa mwendo wa gari.
European cars you can feel the vibe n strength within it... Japanese unaniona kabisa kuna kitu kinamiss
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…