Toyota IST au Toyota Altezza

MAMU35

Member
Joined
Feb 6, 2011
Posts
63
Reaction score
6
Naombeni ushauri kati ya toyota IST na Toyota ALTEZZA ipi ni bora? Hasahasa kwenye uimara na matumizi ya mafuta.

Nasubiri ushauri wenu.
 
Mkuu hizi gari ni two extremes.
Ist ni cc 1300 and 1500. Alteza ni cc 1980 kwenda juu.
Kwa hiyo hata mafuta ni watu wawili tofauti kabisa.
Nyingi za alteza ni gx110.
Budgetwise pia ni tofauti sana nikimaanisha alteza ni muziki mkubwa.
Tastewise na kama unapenda magari. Alteza would be nice if budget is not a constraint
 
Gari zote ni imara, matumizi makubwa ya mafuta ni alteza Kwa spid ndogo, ist ni frugal Kwa spid ndogo, Kwa spid kubwa kinyume chake ni sahihi
 
Sorry samahani kwa kuvamia uzi,na mm nina in between kati ya kununa Rav 4 kilotime na harrier,mwenye maujuzi tafafhari naomba ushauri
 
Angalia nafasi yako ktk space ndani ya Car na Comfortability..., Ni muhimu sana.
Engines za 1GE, ni nzuri kw matumizi ya Mafuta. GX 100, Altezza etc. hutumia Engines aina hizo.
 
Alteza ni nyepesi kufumuka diff kwasababu zipo chini sana

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
Chukua tu IST maana 6 mil sidhani kama utapata Altezza
 
kwa hiyo mpaka kutembea barabarani hiyo toyota ist ninatakiwa kuwa na shilingi ngapi?
Kumbe hujafanya window shopping kujuwa bei ya gari?

kwenye kuagiza gari ni lazima ujuwe bei kwanza ya gari na mwaka uliyotengenezwa then ndio unawrza kufanyiwa makadirio ya ushuru na jumla ya pesa itakayokugharimu in tshillings.
 
Ushauri hapo ni mgumu sana hizo ni gari za jamii mbili tofauti kabisa, Ist mwenzake ni duet, vitz, nissani march, corola, corona, carina etc na Altezza wenzake ni chasser, cresta, verrosa, rav 4, xtrail, tribute etc. IST zipo katika jamii ya low fuel consumption car.
Altezza inakula sana mafuta kama kipato chako ni kidogo hapo si mahali pake, ila IST inakula vizuri wengi wanamuda, baada ya kununua changamoto huwa ni mafuta kuwa makini kuna watu walikimbilia harrier cc 2500 wameishia kuyapaki tu na kuwaonea wivu wenye vigari vidogo.
 
wastani wa fuel cons ni litre moja kwa km ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…