Toyota IST vs Toyota Aqua katika biashara ya Taxi

Sidhani
 
Mzee wako itakuwa anamkubali sana mdogo wako.
 
Wanasema kila mtu na bahati yake!!
 
Itakuwa Story ya INSIDER MAN imemu-inspire sanaaa
 
Nipe 12m nikuuzie Mira, hutajutia. Ina sifa zote... lita moja 27km, ipo juu na ina nafasi... Nini kivule, hii inapanda mpaka milima ya Morogoro...
Anataka second hand from Japan Siyo used from Bongo.
 
Biashara ya Uber pesa unapata ukipunguza gharama za mafuta pamoja na spare. Aqua ya 2015 inatembea 35Km kwa Lita moja tu na kuna watu wanaenda hadi 37Km kwa Lita moja.
Nashauri aende na Aqua hela ataiona.
Tatizo ground clearance ya aqua ipo chini sana,itakuwa ngumu kwa safari za off-road kulinganisha na IST.
 
Elimu yetu inadhalilisha Sana, mtu unamlipia ada mtoto mamilioni mpaka anamaliza, badala aanze kujitegemea inabidi tena wewe ujipange umtafutie mtaji
tena huo mtaji toka kwenya mafao ya baba aliyestaafu utumishi..mzee wake kayasotea hayo mafao miaka zaidi ya 30 kwenye utumishi nae alivyo mjinga asiye na aibu anaona fahari kula jasho la mzee wake alilokusanya toka ujanani..na mbaya zaidi siku kijana akijipata atakula vizuri vyake na mkewe..ila wastaafu nao mizinguo tu wanakumbuka shuka jioooni jua linazama mdo wanaamza kuwekeza.!
 
Kwa uzoefu wangu,hayo magari yenye miaka 20+ hata fuel consumption litakayokupa haiendani na unachokusoma online,hizo takwimu ni za magari mapya!!

NB:Ni raha sana kuendesha gari ambalo ni chaguo lako mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…