Toyota IST vs Toyota Aqua katika biashara ya Taxi

Toyota IST vs Toyota Aqua katika biashara ya Taxi

Hapana,

Mimi nimemwelewa dogo kwa nini amechagua hii Biashara ya taxi. Lengo ni kutengeneza connections.

Kwenye hii kazi unakutana na watu mbalimbali wenye exposure tofauti,business owners,HR's,CEO's nk,hivyo akiitumia kama chance kuna uwezekano wa kumpeleka kwenye stage nyingine. alAnaweza kufanikiwa.
Sidhani
 
Habari wakuu,

Kuna huyu mdogo wetu kitaani hapa amemaliza chuo miaka kadhaa iliyopita ila yupo home Hana mishe za kueleweka. Sasa Mzee kastaafu na ameshachukua kiinua mgongo. Dogo amemwomba Mzee anunue gari ili awe anapiga mishe za taxi mtandao(Uber,bolt nk).

Chaguo lake yeye lilikuwa ni Toyota IST,lakini Mimi nikamshauri achukue toyota Aqua maana ni hybrid car Ina ulaji mzuri wa mafuta inaenda hadi 30km/h hivyo kwa Biashara ya taxi itakuwa nzuri kuliko IST.

Hilo lilikuwa pendekezo langu Mimi.

Ila yeye akaja na hoja kadhaa ambazo ni kama amenichallenji nimeshindwa kutetea hoja yangu.

Hoja zake anasema;

1.Aqua imekaa kimayai haiwezi kuhimili shida na routes za off-road kulinganisha na IST. IST anazikalisha gari nyingi mdogo kwenye hili ikiwemo na hii gari yangu niliyoipendekeza. Anasema IST gari ngumu haiwahi kuchakaa hasa ukizingatia itakuwa inapiga kazi karibia Kila siku,hivyo akaikataa gari Aqua katika hili.

2. Ground clearance.

Anasema Aqua ipo chini sana kulinganisha na IST,hivyo anaiona ni gari ya kwenye lami pekee. Akaniuliza vipi nikipata wateja wa bonyokwa na maji matitu niwakatae?

Kwa kifupi dogo ameikataa kabisa aqua na kung’ang’ania IST ingawa kwa hoja zake bado Mimi nilikuwa napendekeza aqua maana ni latest kuliko hiyo IST ya 2001.

Nimeona niletee humu ili kupata maoni tofauti kutoka kwa wajuzi na wataalamu wa magari,maana Mimi siyo mjuzi wa hilo eneo,japo nimempa ushauri dogo.
Mzee wako itakuwa anamkubali sana mdogo wako.
 
Watu wanazeekea kwenye kuendesha hizo tax mpaka miaka 40 anafanya hiyo kazi hizo connection hazipati ndogo ndo anazipata tu, hiyo ni assumptions mbovu sana, clients wengi hataki kusemeshwa wakiwa kwenye tax sasa huyu dogo wako atakua anawahoji tu kweli atawexa hiyo kazi bila kupata ajali?
Wanasema kila mtu na bahati yake!!
 
Watu wanazeekea kwenye kuendesha hizo tax mpaka miaka 40 anafanya hiyo kazi hizo connection hazipati ndogo ndo anazipata tu, hiyo ni assumptions mbovu sana, clients wengi hataki kusemeshwa wakiwa kwenye tax sasa huyu dogo wako atakua anawahoji tu kweli atawexa hiyo kazi bila kupata ajali?
Itakuwa Story ya INSIDER MAN imemu-inspire sanaaa
 
Biashara ya Uber pesa unapata ukipunguza gharama za mafuta pamoja na spare. Aqua ya 2015 inatembea 35Km kwa Lita moja tu na kuna watu wanaenda hadi 37Km kwa Lita moja.
Nashauri aende na Aqua hela ataiona.
Tatizo ground clearance ya aqua ipo chini sana,itakuwa ngumu kwa safari za off-road kulinganisha na IST.
 
Elimu yetu inadhalilisha Sana, mtu unamlipia ada mtoto mamilioni mpaka anamaliza, badala aanze kujitegemea inabidi tena wewe ujipange umtafutie mtaji
tena huo mtaji toka kwenya mafao ya baba aliyestaafu utumishi..mzee wake kayasotea hayo mafao miaka zaidi ya 30 kwenye utumishi nae alivyo mjinga asiye na aibu anaona fahari kula jasho la mzee wake alilokusanya toka ujanani..na mbaya zaidi siku kijana akijipata atakula vizuri vyake na mkewe..ila wastaafu nao mizinguo tu wanakumbuka shuka jioooni jua linazama mdo wanaamza kuwekeza.!
 
Back
Top Bottom