Toyota Land Cruiser V8 Amazon Ushuru umekua mkubwa kuliko bei ya gari

Toyota Land Cruiser V8 Amazon Ushuru umekua mkubwa kuliko bei ya gari

Tatizo sio V8 bali ni mwaka boss
Gari la 2008 lazima ubamizwe kodi kubwa maana limeekula wese sana ( limekula chumvi)
Hebu angalia la 2018 ulinganishe ushuru huenda ikawa chini
Kwa hiyo uagize hiyo ya 2018 huku ukicheka
 
Wataalamu wa magari naomba kuuliza, "hivi siwezi kununulia gari bandari ya Kenya ili ushuru upungue,kukwepo huo utapeli
Ukiingia na gari kwenye mpaka wa tanzania hata ukanunue uganda itabidi ulipe kodi yote, hata ukinunua znz tu ukifika bara unapigwa difference ili ifanane na kodi ya bara
 
Wakati nipo mdogo tuliambiwa ushuru ni nusu ya bei ya gari.

Ni kweli zama hizi zilikuepo? Mfano gari umeagiza kwa 9M ushuru ni 4.5M?
 
Sema ndinga imekaa kimamlaka kuzidi hata hizi mpya za 2025
Screenshot_20241016-094724.jpg

Hatali mzee kama hii million 28.2 Hadi bongo ila ushuru daha watakichua almost 30 million bado Bandali na mtu watu wakulitoa bandalini hii ngoma Hadi mkononi uandae 65 million wakati Japan million 28 inamana ukiwa Japan hizi gari unanunua 2 kwa hiyo pesa
 
Habari wakuu hivi Kuna namna ya kufanya discount ya Ushuruu? Nahitaji kuagiza hii chuma ila Ushuruu umeipiku Hadi bei ya Gari

Kuna vitu hii nchi ukitizama vizur unaona kabisa kuna mambo yamekaa kiwizi wizi kuna haja gani gharama hizo za kodi kuwekwa kwa mfumo wa USD wakati tuna sarafu yetu ya TSH. Wakati huo gari inatoka Japan na wala sio USA?

Haya ndiyo mambo bunge linatakiwa liyaone na kuyasemea bungeni yabadilishwe.
 
TRA ndo wanafanya hii nchi iwe dumping place kwa kuongeza kodi nyingi hivyo kupelekea watu kununua gari za mwaka 2008 kurudi nyuma
 
Back
Top Bottom