Nunua Toyota,
Sababu kubwa kwanza ukitaka kuuza ni rahisi,ila Nissan Serena utatamba nayo hata milioni moja hakupi mtu.
Kuna jamaa ana mwaka wa pili anaiuza na hamna anaeitaka hata kuiona.
Nissan tatizo lake kubwa ni kwamba mafundi wengi wanazibahatisha hizi gari,sasa unaweza kukuta tatizo dogo unaiweka ndani,na pia spare zake ghali sana na nyingi haziingiliani kama zilivyo Toyota.
Na Pia fuel consumption ya Noah liteace ipo vizuri.
Halafu Noah ni gari bora kabisa ya kizazi cha sasa as Family vehicle,yaani hata kama ukiwaambia wanao wachague basi watachagua Noah.Ninakuambia hivyo kwakuwa ndio natumia kama Family Vehicle.Noah heshima kati ya gari za familia kwa sasa hasa wenye kipato cha chini kama mie,kwanza matengenezo na kesi za kijinga huwa hazina,ila Nissan utajuta mkuu.
Naungana na jamaa hapo kwamba tafuta noah ya chini ya mwaka 2000 ndio zilikuwa toleo bora kabisa.
Ila kuwa makini sana zipo Noah nyingi watu wanachomekewa wakati ni Four wheel Drives,inabidi uulizie vizuri,matoleo ya four wheel drive yatakutesa sana hasa kwenye mafuta ni balaa.Niliona mtu aliagiza Noah na kujua zote ni two wheel drives basi watu wakamletetea kumbe four wheel cha moto anakiona.Na watu wengi sana tusiojua magari tunapigwa kwa style hiyo.
Mie siku zote huwa naona bora niwe mshamba ila lazima niulize mafundi wazoefu kwa ushauri zaidi