labda hapo nikufafanulie kidogo hizo aina ulizozitaja zina maana gani
hizi gari zilitoka katika makundi mawili liteace noah na townace noah, hivyo hizo road tour, g exerb,extra limo,road tour zipo ndani ya hayo makundi mawili nilioyataja.
sr na cr hii inawakilisha code ya aina ya mafuta ambayo gari inatumia ikiwa sr ni ya petrol na cr ni ya diesel. namba mbele ya herufi zinawakilisha drive ya gari 40 ikiwakilisha 2wd na 50 ikiwakilisha awd.
noah ya petrol ina 1998cc wakati ya diesel ina 2184cc
kwa ukubwa wa body liteace zimezidiwa kidogo ukubwa na townace
sasa linapokuja uchukue ipi kwa maoni yangu
1.kifaumbele ipe isio awd kwasababu kama ulivyosema kutoka beya to dar hivyo njia nzuri 2wd itakufaa kwasababu awd inatumia mafuta juu kidogo ya 2wd
2.tafuta townace na sio liteace
3.chukua yenye siti 8 na sio chini ya hapo ili upate faida
4.ikiwezekana chukua ya diesel, engine ya diesel ni vumilivu sana ukilinganisha na petrol pia diesel bei ipo chini ukilinganisha na petrol pia lita moja ya diesel huenda umbali mrefu kuliko petrol.
5. kuwa makini iyovi