Toyota raum, probox 2004 na succeed

Toyota raum, probox 2004 na succeed

Dadio

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
359
Reaction score
42
1599050893871.png

Wandugu habari, naombeni mnipe ushauri juu ya hayo magari apo juu kabla sjanunua. ushauri wenu nautegemea sana katika kutafuta gari ya kuazia maisha yaani gari yangu ya kwanza. Hata kama kuna jingine nje ya hapo ambalo ni nzuri kwa Mtanzania wa kipato cha chini na mazingira ya kibongo basi mtanishauri pia.

Shukrani
 
Ingawa umelete katika wrong jukwaa, naamini mods wataihamisha sehemu husika. Anyway, inategemea sana na uwezo wako wa kiuchumi jinsi ya kuya'handle hayo magari. ikiwemo gharama za mafuta ambayo inakuwa considered kwa kuangalia cc za gari husika.

Gari ulizotaja zote bei zinalingana lingana na hata cc za injini zake zinafanana lakini kimwonekano Raum ni nzuri kuliko probox. Ingawa kama unataka gari ya kawaida tuu na easy ku'maintain sikushauri uchukue gari yeyote kati ya hizo ulizotaja as kuna gari cheap kuzi'handle zaidi ya hizo na ni nzuri pia zaidi ya hizo ulizotaja.
 
Ndo maaana nikaomba ushauri wa ndugu...ni gari gani ukiacha nilizozitaja hapo juu nzuri ktk maintanance na economical in fuel consuption na spare parts... tafadhali naomba mawazo wandugu....
 
Pia kama unaagiza angalia cc kama unataka more economical anzia cc 1500 kushuka chini
 
Kama unataka Gari yenye nafasi kimtindo chukua raum. Ila Gari kama starlet japo ni ya zamani ila ni nzuri kwa mafuta, services na pia spare. Kwa Gari za kisasa zaidi IST, spacial, na corrola new model zinakufaa japo zitakuwa ghali kidogo
 
all in all Toyota cami is the best among all mentioned sema bei yake ipo juu kimtindo ila upande ma mafuta ni cc1290,ipo juu na ni ngumu xana,ist ni gari za mikocheni, masaki na kwingineko ipo chini sana hutakuwa confortable na hali ya barabara zetu.

Pia ni fupi kwa maana ya kwamba ukitaka kusafiri utakuwa unarushwa rusha kama kitenesi but n way natumia raum ya zamani ni ngumu cc1490 ukilinganisha na raumu ya sasa kwani nayo iko chini na ni mayai zaid!probox sio gari ya kudumu muda mrefu na ni mayai japo zipo mpaka za cc990.

Me nataka niuze raum yangu ninunue cami!ila nimeishi vizuri na raum bila matatizo nina miaka miwili kazi yangu huwa ni kumwaga engine oil,na kubadili oil filter tu.
 
Raum new model inanusa mafuta.kama hujagusa reserve ukiweka mafuta ya elfu 5 unatoka bunju hadi mjini safi kabisa!
mafuta ya elfu 10 bunju-town-bunju bila hofu.

service kawaida tu! Nazungumzia cc 1490
 
Raum new model inanusa mafuta.kama hujagusa reserve ukiweka mafuta ya elfu 5 unatoka bunju hadi mjini safi kabisa!
mafuta ya elfu 10 bunju-town-bunju bila hofu.
service kawaida tu! Nazungumzia cc 1490

Unasemaje kuhusu ule mlango wake wa abiria wa kuburuta hivi kama Noah.
Mimi siupendi, unawahi kubomoka!
 
Back
Top Bottom