Toyota RV4 2007 model 2.4 vs Toyota harrier 2.4 model 2003/7

Toyota RV4 2007 model 2.4 vs Toyota harrier 2.4 model 2003/7

Hizi zinakuwa na engine za 5S na sio vvt-i ni ya kizamani hivyo hii kidogo inakunywa kulinganisha na zenye 2AZ vvt-i kitu kingine cha kuangalia zipo pia zenye 4 cylinder lkn ni 4WD full-time hizi pia zinakunywa na zinakuwa nzito kiasi fulani

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante mkuu naona umenifungua ...5s vs 2AZ ,na 2W vs 4W kwa maelezo hayo 2AZ 2W ndo safi and very economical.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi zinakuwa na engine za 5S na sio vvt-i ni ya kizamani hivyo hii kidogo inakunywa kulinganisha na zenye 2AZ vvt-i kitu kingine cha kuangalia zipo pia zenye 4 cylinder lkn ni 4WD full-time hizi pia zinakunywa na zinakuwa nzito kiasi fulani

Sent using Jamii Forums mobile app
maelezo murua kabisa mkuu. Ila kwa nyongeza RAV4 za mwaka 2006 na kuendelea (sina uhakika na kama za mwaka 2005 zina hii feature) 4WD yake ni automatic. ukibonyeza kitufe kuweka on itakuwa on mpaka gari ikifika spidi ya km arobaini kwa saa baada ya hapo 4WD inakuwa disenganged automatically (inajizima yenyewe) bila ya wewe kufanya chochote. Pia 4WD itakuwa disengaged kama ukikanyaga breki kabla ya hiyo spidi 40 kwahiyo ulaji wa mafuta kwa sababu ya 4WD kwa model hizi inakuwa sio ishu
 
mkuu poa kuhusu vvt-i
Nimeambiwa vvt-i 2AZ zinakunywa sana mafuta nataka kuinunua kwa safari za mbali na nje ya Nchi mara kwa mara naomba ushauri kabla sijanunua kwa wenye uzoefu na gari hizi.
 
Nimeambiwa vvt-i 2AZ zinakunywa sana mafuta nataka kuinunua kwa safari za mbali na nje ya Nchi mara kwa mara naomba ushauri kabla sijanunua kwa wenye uzoefu na gari hizi.

zinakunywa sana ukifananisha na nini, mimi nmetumia sana 2AZ engine vvti inalikuwa inatembea km 10-12 kwa lita, so kwangu mimi naona ni economical sana. sasa sijajua unaifananisha na engine gani
 
Performance ya six na four zipo tofauti
Wengi wetu wakiona HARRIER wanajua ndio hio hio lkn machine zinatofautiana
Hawa wajapan wajanja saana walileta landcruiser hardtop engine ni 1HZ(best engine hio) hapo hapo zikaja CRUISER VX FULL OPTION&LUXURY lkn zote ENGINE 1HZ

Sent from Calculator Phone vesion007
Hivi cruiser luxury ina 1 HZ au 1 HDT mkuu
 
Naona watu wengi wanahofia sana gari yenye 4WD kwamba inatumia mafuta mengi sijui watu wanaishije ila gari isio na 4WD ina shida sana ukinasa sehemu umenasa ila inapendeza 4WD ikiwa kwenye gari ilioinuka juu mfano Prado, Surf, Land Cruiser ila 4WD ya kwenye Harrier, Rav 4 ni kujichosha tu
 
Sawa lakini kwenye harrier na rav4 ni All wheel drive (AWD) full time. 4wd kwenye hayo magari mengine uliyoyataja inakuwaga ni optional na unaweza ukaishift gear lever kivyake yani 4wd High, Low, au 1, 2 hii ni nzuri maana ni ondemand haili mafuta.
 
Back
Top Bottom