Toyota RV4 2007 model 2.4 vs Toyota harrier 2.4 model 2003/7

Ahsante mkuu naona umenifungua ...5s vs 2AZ ,na 2W vs 4W kwa maelezo hayo 2AZ 2W ndo safi and very economical.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
maelezo murua kabisa mkuu. Ila kwa nyongeza RAV4 za mwaka 2006 na kuendelea (sina uhakika na kama za mwaka 2005 zina hii feature) 4WD yake ni automatic. ukibonyeza kitufe kuweka on itakuwa on mpaka gari ikifika spidi ya km arobaini kwa saa baada ya hapo 4WD inakuwa disenganged automatically (inajizima yenyewe) bila ya wewe kufanya chochote. Pia 4WD itakuwa disengaged kama ukikanyaga breki kabla ya hiyo spidi 40 kwahiyo ulaji wa mafuta kwa sababu ya 4WD kwa model hizi inakuwa sio ishu
 
mkuu poa kuhusu vvt-i
Nimeambiwa vvt-i 2AZ zinakunywa sana mafuta nataka kuinunua kwa safari za mbali na nje ya Nchi mara kwa mara naomba ushauri kabla sijanunua kwa wenye uzoefu na gari hizi.
 
Nimeambiwa vvt-i 2AZ zinakunywa sana mafuta nataka kuinunua kwa safari za mbali na nje ya Nchi mara kwa mara naomba ushauri kabla sijanunua kwa wenye uzoefu na gari hizi.

zinakunywa sana ukifananisha na nini, mimi nmetumia sana 2AZ engine vvti inalikuwa inatembea km 10-12 kwa lita, so kwangu mimi naona ni economical sana. sasa sijajua unaifananisha na engine gani
 
Hivi cruiser luxury ina 1 HZ au 1 HDT mkuu
 
Naona watu wengi wanahofia sana gari yenye 4WD kwamba inatumia mafuta mengi sijui watu wanaishije ila gari isio na 4WD ina shida sana ukinasa sehemu umenasa ila inapendeza 4WD ikiwa kwenye gari ilioinuka juu mfano Prado, Surf, Land Cruiser ila 4WD ya kwenye Harrier, Rav 4 ni kujichosha tu
 

Sawa lakini kwenye harrier na rav4 ni All wheel drive (AWD) full time. 4wd kwenye hayo magari mengine uliyoyataja inakuwaga ni optional na unaweza ukaishift gear lever kivyake yani 4wd High, Low, au 1, 2 hii ni nzuri maana ni ondemand haili mafuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…