Jamani wanajamvi Mambo vipi.
Msaada, ninakigari changu Aina ya VEROSSA kilikuwa kinazingua mis mis, nkakipeleka KWA gereji, wakamwaga Hydrolic na kuweka nyingine lakini haikusaidia, Mara ikagoma kabisa gia kuingia sio kwenda mbele Wala kwenda reverse haitembei kabisa.
Tatizo ni gia box au engine!?
Je nibadilishe gia box mpya!?
Ushauri please
Inasikitisha lakini nimecheka kwa sauti..[emoji28][emoji28]
Hii ndiyo Tanzania, na mafundi wetu ndiyo hao watanzania wenzetu..
Injini ina miss fundi anabadilisha hydeolic kwa gear box,? kweli..?
Mafundi saa nyingine muwe serious..
Naomba niseme hivi..
1...Baada ya kubadilisha hydrolic inawezekana fundi kaweka hydrolic ambayo si compatible na gear box yako...kwa sababu watu wanadanganyana kuwa Toyota hazizingui huwa zinawekwa hata mafuta ya Korie....kitu ambacho si kweli..
2..Pili, inawezekana gearbox yako ilishafikia mwisho wa maisha, automatic gearbox huwa zina clutch nyingi sana..zikishachoka huwa zinasagika na baadhi ya particles zake zinachanganyika kwenye hydrolic, hapo gari linaweza kubadilisha gear mpaka pale gear box itakapojifia yenyewe...gear box yenye hali hii ukiweka ATF mpya tu, kwisha habari yake kwa sabau ATF ya zamani itamwagwa ikiwa na zile particles zote za clutch.....najua watu watabisha ila siwalazimishi kuamini..(Ukuona halii hii inatokea jua wazi hukuitunza gear box yako au ulikuwa huifanyii service kwa wakati na kwa kutumia geanuine ATF.
3..Tatu, yawezekana solenoid inayotumika ku"shift gears imepata hitilafu....
4....Yawezekana tu wakati fundi anabadilisha ATF alichokonoa may be waya fulani hivyo ikute umeme haufiki kwa gear box yote..
Tuombe Mungu gear box yako iwe imekumbwa na tatizo namba 1 hapo juu B kwa sababu ni rahisi kufix,
Tatizo namba mbili ni gharama sana bora ununue gear box used
Tatizo la miss kwenye engine linaweza kusababishwa na..
1...spark plug mbovu
2... ignition coil mbovu au waya za kuoeleka umeme kwenye coil/plug
3...injector mbovu au iliyoziba
4...mojawapo ya intake valve ikute haifunguki vizuri..
5... lakini pia MAF sensor ikaguliwe vizuri....kadude kana mbwembwe haka kakizingua
Na vijisababu vingine kibaaaoooo
Fanya diagnosis.....Huenda huyo kenge wakati anabadilisha ATF alichokonoa nyaya za solenoid
Tafuta fundi mjuzi atakutatulia shida zote na gari litatembea