Toyota Voltz Vs Toyota Isis

24th DECEMBER

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2013
Posts
401
Reaction score
167
Mwenye ufahamu na magari haya ya aina mbili naomba msaada tafadhali.
Ipi gari bora (uimara na kutulia barabarani)
Toyota Isis &
Toyota Voltz
Ahsante
 
Ni mm mwenyewe ndio siyajui haya magari au tupo wengi... wadau hebu njooni
 
Mwenye ufahamu na magari haya ya aina mbili naomba msaada tafadhali.
Ipi gari bora (uimara na kutulia barabarani)
Toyota Isis &
Toyota Voltz
Ahsante

Chukua voltz utafurahia maisha,tena chukua ile yenye 4WD.iko vizuri mkuu ni mbadala wa Rav4
 
Voltz ziko vizuri zaidi kama walivyosema wadau hapo juu. Wasiwasi wangu juu ya gari hizi ni upatikanaji wa body spare parts kama taa, bumper nk kwani uzalishaji wa hizi gari ulishasitishwa kitambo. Pia niliwahi kusikia kuwa zilitengenezwa pieces 10000 tu.
 
Nimekupata mkuu
 
Chukua toyota isis mkuu, nmeiendesha mara nyingi iko na ukumbi wa kutosha ndani, very comfortable and fuel efficient...Engine yake ilikuwa vvt-i yenye cc1794. Huwa ziko chini so utahitaji kuinyanyua kama utakuwa unakaa maeneo yenye road mbovu!
It has a more appealing body and design kuliko voltz. 24th DECEMBER
 

Ndio mkuu, General Motors ya USA na Toyota ya Japan walitengeneza hizi hatchbacks 10,000 tu mwaka 2002 hadi 2004, ikawa replaced na Toyota Auris. Mkuu, kuhusu spare especially body parts ni kweli zinaweza kua tatizo ila kuhusu internal parts/engine parts zinaingiliana na corolla nyingi tu kama Allex,Run X, corolla X etc.



TOYOTA VOLTZ
Voltz kama alivosema mdau ni 4WD car yenye 1.8L 1.8 L 2ZZ-GE I4 or 1.8 L 1ZZ-FE I4 engine zinazo generate 188hp @7600rpm, hivyo ata mkiwa watu 5 kwenye gari inapiga fresh tu ata milimani.

Ndani ni comfortable sana na ina room ya kutosha kwa kukaa watu na mizigo pia.

Faida ya Voltz dhidi ya Isis
  • Ina power kubwa 188hp dhidi ya Isis mwenye 155hp. Effect yake huwezi notice katika daily driving experience, ila siku mkiwa mmepanda let's say watu 5 wazima, kwenye muinuko utaona moja inavo-enya.
  • Milango ya Voltz ni ya kawaida inafunguka kawaida tu, ila Isis inaslide kama Raum au Noah. Sio kila mtu anapenda hizi.


TOYOTA ISIS
Toyota Isis ni Minivan either FWD au 4WD car yenye engine ya 1.8L 1ZZ-FE I4 au 2.0L 1AZ-FSE I4 zinazogenerate power ya 155 @6000rpm iliotengenezwa tokea mwaka 2004 hadi sasa.

Faida za Isis dhidi ya Voltz
  • Ina machaguo either 1.8L au 2.0L engine sio kama Voltz unapata 1.8L tu, pia unaweza chagua either FWD au 4WD wakati Voltz ana 4WD tu (Sio wote wanaogopa engine size kubwa na wala sio wote wanapenda 4WD engines)
  • Full tank yake kubwa kidogo, ni 60L wakati Voltz ana 50l tu.
  • Ni kubwa kidogo kwa Voltz na inaweza accomodate watu wazima 7, ila Voltz ina accommodate watu 5 tu.


Toyota Isis picha






Toyota Voltz Picha





 

Mkuu voltz zipo za 2WD
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…