Tozo bado ni mwiba kwa Watanzania

Tozo bado ni mwiba kwa Watanzania

Frank Rugwana

Member
Joined
Sep 28, 2022
Posts
6
Reaction score
3
Gharama za maisha zimekuwa zikipanda siku hadi siku. Vyakula vimekuwa juu kiasi kwamba wananchi wanalazimika kuishi maisha magumu kupindukia. Serikali imeshindwa kuwasaidia wananchi ktk kipindi kigumu wanachopitia haswa kuzuia mfumuko wa bei wa vyakula na bidhaa.

Serikali inatambua wazi kuwa hiki ni kipindi kigumu wananchi wanapitia na bado wakaja na tozo ambayo hazina uwazi na uwajibikaji wa matumizi yake.

Wakati watanzania wanaumizwa na tozo gharama za uendeshaji wa Serikali zinazidi kuongezeka bila huruma, viongozi wanazidi kula maisha.

Ni ajabu hata wabunge ambao ndio wawakilishi wetu wamekubali hili wakijua linawaumiza watanzania masikini.

Wabunge wangeambiwa wanatakiwa kupunguziwa mishahara na posho zao zikatwe tozo wangekubali? Kwanini wasiwe mfano kuonesha kuumia kwa pamoja?

USHAURI: Tozo itumike kuchangia bima ya afya kwa kila mwananchi ili matumizi yake yamsaidie mtanzania kwa uwazi. Watanzania wengi wanakufa kwa kukosa huduma za Afya; wananchi wanalia na tozo kwasababu hazina uwazi wa matumizi yake moja kwa moja pia haizingatii haki kwasababu sio maoni ya kidemokrasia.

Hatukubaliana na watanzania juu ya uchangiaji huu, sababu hii ndio chanzo cha malalamiko ya watanzania.

Serikali iache ubabe, turudi mezani tukubalianeni.
 
Niwe tu mkweli; ikitokea 2025 kukawepo na uchaguzi mkuu wa haki na huru, basi CCm itapata pigo kubwa sana.

Inawezekana kuliko hata lile pigo la 2015.
 
Mwananchi gani amekuambia kuwa Tozo ni mzigo? Wakati sisi wananchi ndiyo tuliishauri serikali watuwekee tozo kubwa.
 
Back
Top Bottom