TOZO|CORONA: Idadi ya watali nchini imepungua kwa 77%, Mapato yatokanayo na utali yameshuka kwa 87%, Je mnaopinga tozo hadi leo mnalijua hili?

Pamoja na upungufu mkubwa hivyo wa mapato uliosababishwa na ugonjwa wa Corona mbona serikali haipunguzi matumizi yasiyo ya lazima. Hizo V8 zinatumia mafuta kiasi gani kwa siku nchi nzima? Misafara mikubwa ya viongozi wa kisiasa kwa pesa za serikali je? Rais inatakiwa aongoze kwa mfano kwa kukubali nae alipe kodi kwenye mapato yake ya mshahara nk.
 
Ndugu yangu mimi natumia bando la chuo na naweka mara moja kwa wiki.

Haya mambo ya kujiita sisi ni donor country ni kuumiza tu walala hoi.Kama Kenya wanapokea misaada kibao ya UVIKO kwa nini sisi tukatae.Kuendelea kukamua walala hoi kwa kupitia tozo ili kufidia kupungua kwa mapato ya utalii ni kuzidi kuongeza umaskini.
 
Kenya wa
Wanakopokea hiyo misaada wananchi wanasemaje? Masikini hakombolewi na misaada bro, kamwe haiwezekani. Masikini anakombolewa na juhudi zake mwenyewe.

wangapi unawajua walikuwa choka mbaya lakini leo ni habari nyingine tena bila hata mkono wa mzungu katikati? Tumejilemaza sana, wazungu waje sawa lakini kama partners sio donors.
 
Wewe ni mjinga? Kwani unafikiri sie vyanzo vya mapato au mapato yetu yameongezeka. Watu wenu ni maskini na jobless, waboresheeni maisha na vipato vyao, then leteni hizo tozo hata mara nne ya hizi.
Unakumua pasipo malisho, maana yake mchungaji hayuko serious na kazi yake. Mwisho wa siku hata maziwa kidogo ya kupandia Airbus kila siku kama ilivyoa ada, atayakosa kabisa.
 
Kwa hiyo unaunga mkono tozo zidumu na kodi katika bia ipungue?
 
Wananchi hawana shida na Tozo,Ila wanataka kujua kwanini leo Tozo, Mbona Mwaka jana hazikuwepo,

Kongole nyingi kwa mleta mada,

Tunahitaji kuwa na serikali inayowajibika kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa maelezo ya kina kwani hiki leo sio jana,

Kazi iendelee kiroho safi, Ila muwe mnasema,
 
Unaweza kutueleza kwanini juzi mlipokea ule Mkoppo wa ujenzi barabara vijijini , huku mnaendelea kukata Tozo?

Hata watalii waje wafike billioni hapoa bongo hamna akili za kutumia pesa kwenye maendeleo zaidi ya kujaza hizo pesa kwenye posho na bajeti zenu za mafuta na vikao visivyo na maana wala kichwa.

Endeleeni kula jasho la Wananchi muda ukifika zitawatokea puani hizo.
 
Samia ni mtu anamwogopa Mungu,

Hata tu kupata taarifa za kweli kwamba wataali hakuna tusingeweza kujua,

Tuliaminshwa nchi iko vizuri na uchumi unakuwa kwa kasi kumbe uchumi ulikuwa kwa 2% toka 7%

Tuliambiwa watalii ni kama wote kumbe watalii hakuna,

Binafsi nampongeza sana mama Samia,

Mbele ya Mungu wangu namwahidi kura yangu 2025,

Pamoja na hayo Nashauri Tozo ziendelee tatizo hatukuwa na Taarifa,

Serikali toeni taarifa ,

Sio kutuambia "Vumilieni "

Lazima usema kwanini tuvumilie,
 

..maana yake ni kwamba kuna Watz wengi sana ambao vipato vyao vinategemea sekta ya utalii nao wameathirika kiuchumi na kimapato.

..serikali inayojielewa haiwezi kuongeza tozo au kodi wakati wananchi wake wameathirika kiuchumi au kimapato.

..Na imekosa mapato ya matrillion kutokana na utalii kuporomoka kwanini imekwenda kununua ndege za thamani ya sh trillion 2?
 
πŸ˜πŸ‘πŸ‘ŠπŸ’ͺ
 



Ndio maana wamepunguza matozo karibia mia tatu chifu,

Kilio cha wengi ni sherehe,

Lazima kuwa mzalendo kwa nchi yako otherwise ulegee kwa Mabeberu,

Mimi Samia tu, Tozo kiroho safi kwanza wanaoumia zaidi ni akina Bakresa na akina MO,



Ndio
 
πŸ˜πŸ‘πŸ‘ŠπŸ’ͺ

..mtoa mada amejenga hoja ya kuondoa au kupunguza tozo.

..kama sekta ya utalii na uchumi kwa ujumla umekuwa impacted negatively na janga la corona, basi huu siyo wakati sahihi wa kuongeza tozo au kodi na kuwakamua wananchi.
 
Hizo za watalii uliambiwa wamepewa wananchi wa kawaida ambao mnawaongezea kodi na tozo mara mbili mbili?
 
Ndio maana wamepunguza matozo karibia mia tatu chifu,

Kilio cha wengi ni sherehe,

Lazima kuwa mzalendo kwa nchi yako otherwise ulegee kwa Mabeberu,

Mimi Samia tu, Tozo kiroho safi kwanza wanaoumia zaidi ni akina Bakresa na akina MO,



Ndio

..wametuletea matozo mapya yanayoumiza wananchi.

..kwani serikali imechukua hatua gani za kubana matumizi yake?

..Kubana matumizi ya serikali ndio inapaswa kuwa hatua ya mwanzo kabisa, siyo kuwakamua wananchi.
 
Naunga mkono

Ufungaji MKANDA umekuwa BIAS,wao atujasikia vya kwao vikiguswa na safari hadi za kwenda kufunua VYUNGU pale Kizimkazi.
 
Nakuunga mkono.
Bado hakuna logic ya kuwakata pesa wananchi wa kawaida,hiyo kufunga mkanda ianzie kwa viongozi kwanza kabla haijawafikia raia.
Haiwezekani wakati wa shida hao bado waendelee na maisha yaleyale ya kutumbua pesa kwa safari zisizo na msingi wakitembelea mashangingi.
Hivi umejiuliza kama serikali imeshindwa kupata mapato huyo raia unayemkata tozo anapataje pesa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…