Tozo hadi malipo UN (Umoja wa Mataifa)

Tozo hadi malipo UN (Umoja wa Mataifa)

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
SAMAHANINI, mdogo wangu anafanya kazi Serikalini, amenisumbua nimtumie pesa za matumizi huko DSM alihitaji kununua vitu, nilipomuuliza alienda kufanya nini, akasema alikuwa anafanya shughuli na shirika moja na UN na badala ya kuwalipa malipo ya kiUN, wamewalipa malipo ya kibongo, walipouliza wanaambiwa kuwa SERIKALI HII IMETOA WARAKA KWAMBA WAFANYAKAZI WA SERIKALI WAKIFANYA KAZI NA UN, WANATAKIWA KUPATA PERDIEM ZA KIBONGO.

Nafahamiana na watu kadhaa wanaofanya kazi UN wapo hapo DSM, niliwapigia kuwauliza jambo hili, wamenithibitishia kwamba ni kweli, Serikali hii baada ya kutoa waraka mpya wa malipo kwa watumishi, wamesambaza kwa mashirika ya kimataifa kwa maana hiyo, ukifanya kazi na UN ulikuwa unaweza kupata per-diem kwa dola mia mbili kwa mfano, lakini kwasababu ya waraka huo UN wanacomply na inachosema Serikali, watakupatia hata dola mia haifiki.

Cha ajabu, inasemekana UN wanasema wafanyakazi wa mashirika toka nchi zingine za Afrika ambao hawajaweka waraka, wanapokea malipo kwa dola, ila kwa tz pekee. hivyo mfano ukifanya kazi pamoja na wakenya wao watapata malipo ya kiUN na wewe utapata malipo ya kibongo, kwa kazi hiyohiyo.

Sio kwamba UN hawana pesa za kulipa watu, inavyosemakana, UN pia wanalalamika kwanini serikali inabania watu wake? pesa sio za kwao ni za UN, lakini serikali inaumia kwanini watu wake wanazipata? au ndio maana ya tozo hadi kwenye miamala ya UN? ulishawahi kuona mzazi anakataza mtoto wake asipewe za msaada wakati uwezo hana? imeniuma sana kusikia hivyo, yaani ni kwamba serikali ambayo inawapenda watu wake itazuia UN isiwape raia wake malipo ya kimataifa wapewe malipo ya kibongo? and this is confirmed nimethibitisha.

MWENYE HUO WARAKA WA MALIPO YA SERIKALINI PLEASE AUWEKE HAPA. na waziri husika afyatuliwe mbali, au wanafikiri kuwaambia UN wasiwalipe watu pesa za kutosha ndio watapendwa na UN? wapendeni raia wenu, angalieni wakenya wanavyofanya kwa raia wao mjifunze nyie mapimbi.
 
kwamba serikali inaonea wivu hata pesa isiyokuwa yake? pesa watoe UN alafu uwapangie mtoto wako apate shilingi ngapi, inawaumaaaa? au nini sijaelewa.
 
matokeo yake, UN nchi zingine wanaendelea kutoa dola, kwa bongo wanatoa kile serikali imetaka, posho tu. nilishangaa sana kusikia hivyo.
 
Hahah nimecheka hapo mwisho. Hicho ndicho kinachofanyika mtoa mada, ukitaka ulipwe kama wanavyolipwa wao usiwe mwajiriwa wa serikali. Labda uwe vendor au freelancer.
 
Back
Top Bottom