Tozo katika awamu ya 6 imekuwa kawaida, lini gharama za maisha kwa wananchi wa kawaida zitapungua?

Tozo katika awamu ya 6 imekuwa kawaida, lini gharama za maisha kwa wananchi wa kawaida zitapungua?

Big Phil

Member
Joined
Nov 20, 2019
Posts
50
Reaction score
339
Hili neno limekuwa maarufu sana kipindi hiki cha awamu ya 6, lini litafika mwisho na lini gharama za maisha kwa wananchi wa kawaida zitapungua! Mafuta ya kula juu, petroli ndo balaa, mbolea, yaani necessary items zote hazishikiki na bado upatikanaji wa hela umekuwa mgumu sana.

Na wakati huo huo serikali bado wanaendesha miradi mikubwa kama ununuzi wa ndege na kununua magari ya kifahari + matumizi makubwa serikalini kwa gharama za wananchi. Serikali inapaswa kupunguza gharama na ugumu wa maisha kwa wananchi, tusiseme mbona majirani wana gharama za juu za mafuta. Inawezekana lakini kila nchi ina vipaumbele vyake kwa watu wake. Inawezekana jirani zetu wana uchumi mzuri, uzalishaji mzuri wa chakula na huduma bora za afya na elimu bora, au na wao wana matatizo yao kama political instability.

Sisi watanzania tumebarikiwa rasilimali nyingi sana ikiwemo rasilimali watu zaidi ya Milioni 60, Madini ya kila aina, Ardhi nzuri inayofaa Kwenye kila aina ya Kilimo ambayo jirani zetu hawana, tuna vivutio vingi vya kitalii Serengeti national park, mlima kilimanjaro, Ngorongoro nk. Viongozi wetu waje na njia nzuri ya kutumia hizi maliasili ili iweze kunufaisha uchumi wa nchi na sio kutegemea wazungu kutuamulia uchumi wetu.
 
Back
Top Bottom