Kila nchi duniani hukusanya kodi kutoka kwa wananchi kwa ajili ya kuendesha serikali, na kodi ni chanzo kikuu cha mapato ya serikali.Lengo kuu la kodi ni kwaajili maendeleo ya nchi kwa maana kujenga huduma za kijamii kama shule hospitali, barabara, huduma za maji,reli na kadhalika.
Katika nchi yeyote ile lazima wananchi walipe kodi ili kuchangia maendeleo na kulipa kodi sio hiari ni lazima ndio maana ,Ili kodi iwezwe kutozwa lazima kwanza itungwe sheria na bunge ndipo kodi ianze kutozwa kwamba haiwezi kuwepo kodi bila kuwa na sheria.Sheria zote zinapitishwa na bunge hata sheria za kodi nazo zimepitishwa na bunge, sheria ya tozo kwenye miamala ya simu, kwenye mabenki, nakadhalika ilipitishwa na bunge.
Na bunge ndio lenye jukumu la kupitia muswada wa sheria ili kujiridhisha kama muswada unafaa kuwa sheria ama haufai. Hivyo basi ,malalamiko yeyote yale kuhusu tozo ambazo tozo hizo zipo kwa mujibu wa sheria ambazo zilipitishwa na bunge, watu wa kwanza kulalamikiwa wanapaswa kuwa wawakilishi wa wananchi.
Pamoja na dhamira nzuri ya serikali ya kuanzisha tozo hizi kwa lengo la kuboresha huduma mbalimbali za jamii kama, kujenga vituo vya afya,tozo hizi kusaidia kutoa elimu bure, mikopo elimu ya juu, kutoa ruzuku kwenye mbolea lakini bado tozo hizi zinazidi kumpa mzigo na ugumu wa maisha mwananchi mwenye kipato cha chini.
Na kilio kikubwa kwa wananchi katika kipindi hiki ni kupanda kwa gharama za maisha ambazo zimechangiwa na kupanda kwa bei ya mafuta, kupanda kwa bei za vyakula, kupanda kwa nauli na hivyo gharama za maisha kuwa juu. Katika mazingira haya wananchi wengi hawakutegemea kuongezewa gharama nyingine tena ya tozo,ambayo tozo hiyo inagusa moja kwa moja maisha ya mwananchi na hasa mwananchi mwenye kipato cha chini.
Tozo hizi zinaathiri uwezo wa wananchi wa kipato cha chini kujiwekea akiba, zinaathiri uwezo wa kufanya uwekezaji mdogo mdogo, pia zinaathiri uwezo wa mwananchi kufanya matumizi kama zamani mwananchi wa kipato cha chini aliweza kununua mahitaji ya chakula kwa shilingi elfu mbili na kwa sasa hawezi kununua mahitaji hayo, basi tozo hizi zimeathiri moja kwa moja maisha ya mwanchi wa kipato cha chini.
Kitendo cha kuweka tozo kwenye miamala ya simu na miamala ya kibenki kwa kiasi fulani inakiuka sera ya mfumo wa fedha jumuishi(financial inclusion policy) ambayo inataka idadi kubwa ya wananchi watumie mifumo rasmi ya kifedha badala ya mtu kuweka fedha kwenye kibubu basi angeweza kuweka kwenye mfumo rasmi wa kifedha ambayo makampuni ya simu kupitia miamla ya simu ilikua ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya mfumo wa fedha jumuishi.Ni wazi kwamba asilimia kubwa ya watu wa vijijini na fedha zao kwa kiwango kikubwa zilikua zinatunzwa kwenye simu za mkononi, kuongezeka kwa tozo kunasababisha watu warudi kwenye mfumo wa zamani wa utunzaji wa fedha ambao ulikua unachochea uhalifu.
Ili kupunguza gharama za maisha kwa wananchi hasa katika kipindi hiki ambapo kuna mfumuko wa bei katika bidhaa mbalimbali ambazo ni za lazima kwa mwananchi, Serikali itumie wataalamu wake wa ndani kubuni vyanzo vingine vya mapato vya kudumu ambavyo vitaongeza idadi ya walipa kodi na kumpunguzia mzigo wa kodi na tozo mwananchi wa kawaida.
Ni jukumu la serikali kutengeneza tabaka la wafanyabiashara wengi ambao watalipa kodi badala ya hizi tozo ambazo zimekua mzigo mkubwa kwa mwananchi wa kawaida.
Aidha serikali inaweza ikaingia kwenye uzalishaji kwa mfano ikatengeneza meli za uvuvi kwenye bahari na maziwa yaliyopo nchini kwani kuna ukanda wa bahari kutoka Tanga mpaka Mtwara, ambapo bahari ile bado haijatumika vizuri hasa katika upande wa uvuvi,serikali inaweza kutengeneza meli za uvuvi za serikali na serikali ikavua samaki ikauza ndani ya nchi na nje ya nchi na ikawa chanzo kikubwa cha kudumu cha mapato na kumpunguzia mwananchi wa kawaida mzigo wa tozo.
Aidha katika bara la Afrika Tanzania ni nchi mojawapo yenye idadi kubwa ya mifugo, na sekta ya mifugo haijatumika ipasavyo kwenye pato la taifa, kama serikali ingejenga na kuhamasisha wawekezaji wengi zaidi katika sekta ya mifugo, pamoja na kujenga viwanda vingi vya uchakataji wa mazao ya mifugo ili kuongeza mnyororo wa thamani kwa bidhaa zitokanazo na mifugo na hivyo kuchangia katika pato la taifa.
Badala ya kupeleka ng’ombe nchi za nje basi ipelekwe nyama ili kuongeza thamani ya bidhaa na hivyo kupunguza mzigo wa tozo kwa mwannchi wa hali ya chini. Hata hivyo kutokana na nafasi ya kijiografia, Tanzania imezungukwa na nchi nane ambazo ni Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Msumbiji, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Malawi na Zambia, katika nchi hizi ni nchi mbili tu zenye bandari, kwa maana zilizopitiwa na bahari, lakini nchi sita hazijapitiwa na bahari yaani(land locked countries) na zinapitishia mizigo yao Tanzania ingawaje sio kwa asilimia kubwa, Tanzania ina uwezo wa kutengeneza mazingira ya bandari zetu ili asilimia Zaidi ya 90 ya mizigo kwenda nchi hizi ipitie bandari za Tanzania, kwani mizigo yote mikubwa inasafirishwa kwa njia ya maji, na hilo linawezekana kwa kuboresha utendaji wa bandari zetu. Hii itasaidia kuongezza chanzo cha kudumu cha mapato na kupunguza mzigo mkubwa wa tozo kwa wananchi.
Hivyo basi serikali iwekeze zaidi kwenye vyanzo vya kudumu vya mapato ili kuwa na vyanzo endelevu vya mapato vitakavvosaidia katika ukusanyaji mkubwa wa mapato na kuleta maendeleo ya nchi katika sekta mbalimbali. Kwani tozo hasa katika miamala ya simu na mabenki sio chanzo endelevu kwasababu pindi mwananchi akiamua kuacha kufanya miamala ya simu au ya kibenki na kuamua kutumia njia za asili kama kibubu basi serikali itakosa mapato na kukosa namna ya kukusanya kodi hii kwa baadhi ya watu na kukosa namna ya kumwajibishwa kwani sio lazima na wala si kosa kisheria pindi mtu wa kawaida anapoacha kuweka fedha benki au kufanya miamala kwenye simu.

Upvote
6