Lazima wewe utakuwa ni miongoni mwa wajinga ambao wametufikisha hapa tulipo kama Watanzania.
Tatizo tunaliona na tunalijua vizuri sana ila kwa kuwa sote ni sehemu ya tatizo tunatafuta wa kumtupia lawama.
Nchi hii tumejaaliwa mengi sana lakini kuna usemi wa wahenga, a fool and his money are soon parted!
Kwa sababu ya ujinga wetu tumeruhusu udikteta wa kikundi cha watu kwa kivuli cha chama cha siasa.
Hiki kikundi kinaimiliki ardhi yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vyote vilivyomo.
Hiki kikundi kinaimiliki dola na vyombo vyake vyote. Kina hatimiliki ya uhuru, haki na usalama wa raia wote
Ole wako kama wewe si mwana kikundi, au ukijitoa kwenye kikundi hiki, moja kwa moja wewe ni adui wa taifa.
Huwatakii mema hao mawakili wasomi kwani hicho kikundi pia kinamiliki hata haki yako ya kuishi duniani.
Dawa ya kupambana na genge hilo ni sisi Watanzania kwa ujumla wetu na si moja moja au vikundi vidogo vidogo.
Tutafikia ujasiri huo siku tutakapozinduka usingizini na kuondokana na vitu vitatu; ujinga, unafiki na uoga!