Tozo, Miamala, Kikokotoo - Tanzania tuna Wanasheria Wasomi?

Mwanasheria gani mwenye akili timamu ajitokeze kuwa tetea watu wasio jitambua hivi Kuna muda watu mnajitoa ufaham hata wa mambo madogo tu
Sasa hao watu watajitambua vipi kama wasipo elimishwa na hao wasomi?

Wewe bhana kubali tu Tanzania kwa sasa ina wasomi wengi wanafiki na ambao akili zao kwa sehemu kubwa zinawaza uteuzi tu ili na wenyewe waishi maisha mazuri ndani ya siasa, badala ya kutetea wanyonge.
 
Kwa sababu mnachopigia kelele ni kitu genuine na Cha maana ndio maana wanawapuuza na kuwaona wajinga tuu..
Ni sahihi huenda sisi ni wajinga - lkn wasiwasi wangu ni kuwa kundi lenu mnaosapoti hili huenda ni wapumbavu ndiyo maana kila jambo mnakuwa Yesist
 

Tuko tunajadili mambo ya Simba na Yanga, hayo ya tozo hatuna muda nayo.
 

Kama wanasheria na wao wako kwenye mijadala ya kina kajala na Diamondi unategemea nini?
 
Hii Tanzania siyo Kenya.
KIFUPI: Nadhani watakuwa wamesoma upepo, na kutumia mantiki kuwa kama waliotangulia hawakusikilizwa. Je, hizo nguvu za kusikiliza wanasheria zitatoka wapi?
Wananchi wamelalamika Sana juu ya tozo, lakini tuliambiwa kuwa wananchi wanazikubali tozo isipokuwa zipunguzwe.
Mkutano huo wa wananchi waliokuwa wanasema tumezikubali tozo ila zipunguzwe ulifanyikia wapi?
Sasahivi, mwendo ni amri kutoka juu kwenda chini kwa ajili ya kutekelezwa tu siyo kujadiliwa.
 
For sure nina wasiwasi sana kuwa ukimya na utulivu wa watanzania ndiyo chanzo cha kubebeshwa mizigo
 
Tusiufiche uzi huu - wanasheria kuweni mawakili wa wananchi - barabarani kwenu yanapitishwa mambo mengi ya hovyo hovyo.
 
Tusiufiche uzi huu - wanasheria kuweni mawakili wa wananchi - barabarani kwenu yanapitishwa mambo mengi ya hovyo hovyo.
Lazima wewe utakuwa ni miongoni mwa wajinga ambao wametufikisha hapa tulipo kama Watanzania.

Tatizo tunaliona na tunalijua vizuri sana ila kwa kuwa sote ni sehemu ya tatizo tunatafuta wa kumtupia lawama.

Nchi hii tumejaaliwa mengi sana lakini kuna usemi wa wahenga, a fool and his money are soon parted!

Kwa sababu ya ujinga wetu tumeruhusu udikteta wa kikundi cha watu kwa kivuli cha chama cha siasa.

Hiki kikundi kinaimiliki ardhi yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vyote vilivyomo.

Hiki kikundi kinaimiliki dola na vyombo vyake vyote. Kina hatimiliki ya uhuru, haki na usalama wa raia wote

Ole wako kama wewe si mwana kikundi, au ukijitoa kwenye kikundi hiki, moja kwa moja wewe ni adui wa taifa.

Huwatakii mema hao mawakili wasomi kwani hicho kikundi pia kinamiliki hata haki yako ya kuishi duniani.

Dawa ya kupambana na genge hilo ni sisi Watanzania kwa ujumla wetu na si moja moja au vikundi vidogo vidogo.

Tutafikia ujasiri huo siku tutakapozinduka usingizini na kuondokana na vitu vitatu; ujinga, unafiki na uoga!
 
Huenda uko sahihi kuwa mimi ni mjinga lkn kwa kuwa ujinga wangu unalenga kuwapunguzia watanzania mzigo wa rundo la kodi, tozo na Miamala basi huenda niko kundi la wajinga bora.

Sasa wewe mwelevu ungana na wajinga wengi kupinga, kushauri, na kubuni njia za kuondokana na vitu vingi vya hovyo hovyo.
 
Tozo imekuwa topic kwa mda mrefu imewafanya watanzania wasahau kama kuna utalii madini gesi Na bandari
Something is not right
Somebody is playing games
Inaonekana jamaa analipwa vizur tu kwa kuleta taarifa isyo Na faida kwa nchi in the name of tozo
 
Ndiyo maana mimi nashangaa kusikia wanao jihita wasomi kutaka mishahara mikubwa wakati hata kuwalipa laki 2 kwa mwezi ni kuwapendelea sana ...
 
Tuliwaambia msimfananisha JPM na vitu vya kipumbavu vya msoga mkabisha
 
Yupo Profesa Moshi aliesema kuwa waziri asiangalie kodi rahisi rahisi aangalie vyanzo vingine zaidi na kutanua wigo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…