michu03
Member
- Dec 1, 2018
- 72
- 39
Neno Tozo kwa siku za hivi karibuni limekuwa kama wimbo unaoimbwa na kila mtanzania wa kila hali, hivi sasa tozo za maiamala ya simu hata tozo za majengo ni jambo la kuumiza na selikali imetoa tamko la kusisitiza kwamba tozo haziwezi kuondolewa ikiamini kuwa ndio mojawapo ya njia halali za kujiingizia kipato , lakini kiuhalisia watu wengi walioko mtaaniwanaumia sana na kwa siku za karibuni kumekuwa na matabaka kati ya serikali na watu imetengeneza utofauti kati ya serikali na watu inaowahudumia mtaani.
Ni kawaida kwa watanzania kuyafanyia mzaha hata mambo yanayowaumiza ili kujifurahisha imefikia hatua wanalinganisha Neno Tozo na TZ vitu viwili ambavyo hata havihusiani.
Labda niziainishe athari za kiuchumi zinazoweza kutokana na tozo miongoni ni kama zifuatazo:-
Kuzorota kwa biashara matandaoni
Ongezeko la la tozo itapelekea wakati mgumu sana kwa wafanyabiashara walioanza kuchipukia na kutumia mtandao kwa ajili ya kuuza biadhaa pia kufanya malipo mitandaoni.
Mfumuko wa bei za bidhaa na huduma
Kama kuna ongezeko la fedha katika miamala ya simu ni wazi fika kwamba gharama za huduma au bidhaa zitolewazo mtandaoni zitaongezeka kwa wanaofanya miamala. Hivi sasa kuna hatari ya mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali, mfumuko wa bei uko kwenye tarakimu 3.3% na ongezeko la tozo kinaweza kupandisha hali ya mfumuko zaidi.
Mzunguko wa fedha kudorora
Kutokana na kupungua kwa kasi ya huduma ya kutuma na kutoa fedha basi fika kutakuwa na mdororo wa fedha na kufanya hali ya kiuchumi ya mtu mmoja mmoja kuwa ngumu.
Gharama za maisha ya watu zitaongezeka kuzingatia ongezeko la gharama katka huduma mbalimbali wakati pato la mtu mmoja mmoja likiendelea kuwa lilelile ama kushuka kutokana na athari zinazosababishwa na COVID-19.
Kuyumba kwa sekta binafsi kama makampuni ya simu kutokana na kupungua kwa watumiaji ama matumizi (Expenditure) kupungua.
Dhumuni la makala hii ni kujaribu kuziamsha fikra kuona ni kwa namna gani mamlaka husika , wizara yafedha wanaweza kuyatumia mapato yatokanayo na tozo kutengeneza walipa kodi zaidi na wa hiari lakini pia kwa vijana wenzangu kuibadili changamoto hii kuwa fursa ya kibiashara na kujalibu kuziangazia fursa zitokanazo na tozo.
Ningependa nianze na ushauri kwa wizara ya fedha na mipango:
Hivi karibuni Waziri wa Fedha na mipango Dkt Mwigulu Nchemba alitangaza wamefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi za kitanzania Bilioni 48.4 katika kipindi cha wiki nne za mwanzo toka kuanza kwa tozo hizi na wakaanisha matumizi ya fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa miradi inayosimamiwa na serikalilakini pia kuwezesha huduma mbalimba kama afya, elimu, maji n.kLakini moja ya vitu mhimu vilivyo takiwa kufanywa ni kuhakikisha unatengeneza ama kulifanya zoezi hili liwe endelevu ni lazima uwawezeshe wananchi kiuchumi kwani wao ndio walipa kodi, kuwafanya wazimudu gharama za maisha pia kuwekeza katika miradi itakayohakikisha inakuwa chanzo cha mapato, Kuliko kuwekeza kwenye miradi inayoweza kupelekea rushwa na ubadhilifu kwa watendaji na wasimamizi wasiowaaminifu na kuongeza maumivu zaidi kwa walipa kodi.Ingependeza kungekuwa na miradi yenye lengo la kuendelea kuzalisha walipa kodi na kuongeza makusanyo maradufu.
Mfano najaribu kuwaza iwapo wizara ingeamua kufadhili miradi katika maeneo yafuatayo:-Miezi kadhaa iliyopita Soko la Kariakoo Kitovu cha biashara katika jiji la kibiashara lenye muingiliano wa zaidi ya watu milioni 4, JIJI LA DAR ES SALAAM liliteketea kwa moto, Mali za wafanyabiashara ambao kimsingi wengi wao walitegemea biashara zao kuyaendesha maisha yao ya kila siku pia ziliteketea, Ambao ni walipa kodi na wananchi wa kawaida hakuna jitihada za kuwawezesha zikifanyika.
Kwa muda mrefu nimekuwa nikiatafakari Ubora, Miundombinu, Utaratibu na Muundo katika soko hili lenye taswira na umaarufu ukanda wa afrika masharariki haviaksi ushindani kimataifa na kutengeneza mapto zaidi.
Nawaza kama pesa ya iliyopatikana katika tozo ingetumika katika ukarabati na kuboresha miundombinuya kisasa,yenye ubora na inayoweza kudhibiti majanga yanayoweza kujitokeza kama moto, kimbunga, mafuriko nk pia usanifu wa viwango na wakuvutia unaoweza kulitangaza soko kimataifa kuvutia wachuuzi, wawekezaji na watalii afrika hata ulaya.
Kuwezesha matumizi ya TEHAMA katika miundo, utendaji kazi, ukusanyaji mapato, Utunzaji kumbukumbu pia katika malipo na manunuzi. Kuongeza viwango vya utaoji huduma na utaratibu rafiki kwa wateja ambapo wafanya biashara ama watoa huduma walete pamoja na wasomi na wataalamu wa wabiashara kutoka taasisi mbalimbali za elimu na vyuo kuwapa mafunzo maalumu ya kuwawezesha ni jinsi gani ya kuhusianisha elimun na biashara, biashara na uhusiano wa kimataifa, Bajeti, Kuandaa mpango wa biashara , Kuweka kumbukumbu za biashara, Elimu ya kulipa kodi, Kujikinga na majanga , Elimu ya bima na Uwekezaji katika soko la hisa. Baada ya ukarabati na mafunzo kukamilika wafanyabiashaara wanawezeshwa kwa kupewa mitaji ama kukopeshwa, wanpewa uhuru wa kufanya biashara chini ya uangalizi wa tasisi za elimu za biashara na wataalamu ili waendelee kukuza biashara zao.
Kuna faida zinazoweza kupatikana kutokana na mpango kama huu ni zifuatazo:-
- Kuwezesha wakulima na wazalishaji wa bidhaa kupata soko la uhakikika la bidhaa na mazao yao
- Kuongeza ushindani na kutengeneza soko shirikishi ukanda wa kusini mwa jangwa la sahara
- Kusaidia kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja kwa kupunguza mdororo wa mzunguko wa kifedha na kufungua fursa zaidi za kiuchumi, Uwekezaji na utalii na uhusiano wa biashara kimataifa
- Kuchochea uvumbuzi na matumizi ya teknolojiaa ya habari na mawasiliano. Kusaidia kuongeza mapato yatokanayo na tozo zaidi
- Kusaidia kuendeleza miundombinu ya barabara na mawasiliano mfanom reli ya kisasa (SGR).
Ipo mipango mingi inayoweza kushabiana na huu ambayo inaweza kuelekezea mapato yatokanayo na tozo kutengeneza mapato mengi zaidi pia kupunguza tatizo la ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu waliopo mtaani kwa mfano kuanzisha benki ya vijana itakayowezesha kutoa mikopo na mitaji kwa vijana wenye uhitaji wa mitaji kuanzisha makampuni ya usimamizi ya wazawa na serikali kuyagawia tenda makampuni iliyaweze kujiendeleza.
Pia Inawekana kutumia Tozo kuchochea uvumbuzi na matumizi ya TEHAMA ambayo yanaanza kuzorota kutokana tozo kuwa upande wa mtandaoni, kuna biashara za mtandaoni zenye faida zinazohusisha watu wengi Kama E- Commerce, Sarafu za mtandao( Crypto-currencies) na vingine kama hivyo.
Kwa kuhitimisha, ningependa kushiriki na wasomaji wa makala hii baadhi ya fursa zinazoweza kupatikana kutokana na changamoto na kupelekea mawazo ya biashara yenye kutengeneza mapato mazuri waswahili wanasema “Kila baya mbolea”.
Kwa mujibu wa Takwimu kutoka Mamlaka y Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kati ya laini 53.1 millioni zilizosajiliwa kisasa 32.7 Millioni zinatumia huduma za kifedha mtandaoni, Huku Tanzania ikiwa na jumla ya watumiaji 29 Millioni wa huduma za Intaneti. Yanga yam zee mpili wanasema “wana watu” na mimi nataka niseme fursa ama biashara ni watu. Ikiwa serikali imeweza kukusanya mapato ya billion 48+ kwa wiki nne tu za ,mwanzo hii inamaana kibiashara kuna watu wengi sana mtandaoni na Mapato ya biashara ya mtandaoni yanakadiliwa kuwa makubwa sana.
Nataka twende taratibu tikichambua changamoto moja hadi nyingine na njia ya kuitatua, Kutokana na swala hili la Tozo waathirika wakubwa ni makundi yafuatayo:-Makampuni ya simu na benki za mtandaoni, Wafanyabiashara wa mtandaoni, Mawakala ambao wote wanawategemea watumiaji wa huduma za kifedha mtandaoni kama watumiaji wa huduma zao.
Katika dunia ya sasa ya mapinduzi ya nne viwanda biashara za mtandao ya kijamii ya kuuza data, sehemu ambapo makampuni yanaweza kupata watu kutangaza biashara zao mfano mzuri ni facebook, Twitter, Google nk.
Najaribu kuwaza kuwepo na platform inayowaunganisha wateja wa huduma za kifedha wa mtandao w uhakika na makampuni ya simu, wafanyabiashara wa mtandao na mawakala walipie kuwapata wateja hao kulingana na idadi ya wateja katika mtandao husika.Hii inakuwa hivi kunakuwa na namna watu wanajiunga na wanajisajili katika mfumo kwa kujaza taarifa zao mhimu na ni mtandao upi wanatumia kutuma na kupokea fedha ili waweze kutuma na kutoa fedha mtandaoni bure taarifa data hizi zinnauzwa kwa makampuni ya simu kutokana na wateja waliojiunga.
Pia kuna malipo ya awali naya mwezi yatakayotakiwa kufanywa na mawakala na wafanyabiashara ili kulipata kundi hili, lakini pia kunaweza kuwa na namna ya kutengeneza pesa kwa kampuni kulipia kufanya matangazo, kutengeneza application na kuiweka kwenye store kama appstore na playstore.Pia ukiachana na hayo kunaweza kuwa na makampuni ya Tax consultant, kuzishauri kampuni za simu na wafnyabiashara wa mtandaoni na namna ambavyo wanaweza kukabiliana na hali , Pia makampuni mfano wa bima ambapo watu na makampuni yatajiunga ili watume na kupokea fedha bure lakini wanafanya malipo kila baada ya kipindi cha muda( subscription) mfano siku, wiki ama mwezi.Ningependa kumaliza na niwakalibishe watu wenye maoni na namna ambayo tunaweza kuibadilisha changamoto ya Tozo na kuwa kama fursa.
Upvote
3