Mh. Mwigulu anataka kutuaminisha kuwa bila hizo tozo nchi na mipango yote itakuwa grounded, hakuna chanzo kingine cha pesa, hakuna hata pesa hata moja ambayo inapotea lakini tu hazitoshi.Sisi tulishajua nchi hii ina pesa nyingi baada ya hayati JPM kulisisitiza hilo mara nyingi tu enzi za uhai. Yeye hakukusanya tozo lakini bado alisisitiza nchi ina pesa nyingi sana, labda kwa sasa walamba asali wamekuwa wengi kupindukia hali inayopelekea walalahoi wakamuliwe hadi tone la mwisho la damu.