KERO Tozo ya Bajaj Stendi ya mabasi Magufuli: Nani anapaswa kulipa?

KERO Tozo ya Bajaj Stendi ya mabasi Magufuli: Nani anapaswa kulipa?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

cEHO

New Member
Joined
Jan 30, 2024
Posts
4
Reaction score
3
Unapopanda bajaji kwenda Stendi ya Mabasi ya Magufuli, Mbezi, unaambiwa nauli yako inaongezwa Shilingi 500 kama tozo ya kuingia stendi.

Kinachoshangaza ni kwamba tozo hiyo inayotozwa kwa waendesha bajaji inaonekana kulipwa na abiria, badala ya kubebwa na mwenye bajaji ambaye ndiye anayefanya biashara ya usafirishaji.

Tunaomba mamlaka husika itoe ufafanuzi kwa jamii: Je, kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa, nani anapaswa kulipa tozo hiyo—abiria au mtoa huduma wa usafiri?

Wananchi tunahitaji uwazi ili kuepusha tozo kutozwa kiholela na kuhakikisha abiria hawatozwi gharama ambazo si wajibu wao.
 
Back
Top Bottom