Tozo ya majengo inayolipwa kupitia Luku inakatwa kila mwezi au kila ukinunua umeme?

Peramiho yetu

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2018
Posts
5,303
Reaction score
14,983
Wakuu habari za jioni kwa mashabiki wa biashara United timu Bado haijatoka hadi mda huu kwenda Djibouti.

Niende kwenye mada kuu naomba kuuliza wakuu mnisaidie juu hili tuliambiwa kodi hii itakuwa inakatwa kila mwezi lakn maajabu Leo nimenunua umeme naona inakatwa tena hii kodi

Au n Mimi sikuelewa tangazo lao au wameamua kujichukulia sheria zao binafsi

Wakumbuke wengne umeme tunanunua wa 1000 kulingana na vipato vyetu sasa naona wanatulazimisha kinyume na makubaliano tuliyo kubaliana hapo awali

Kwa wanasheria siwezi kuwashtaki hawa Tanesco na wizara ya ardhi naona kama wamevunja makubaliano

Cc TANESCO @Petro E. Mselewa @Pascal Mayalla

Sent from my TECNO F1 using [URL='http://r.tapatalk.com/byo?rid=77694']JamiiForums mobile app[/URL]
 
Leo ni mwezi wa ngani na mwisho ulinunua mwezi upi?

In short mpaka leo inabidi uwe ushakatwa buku 3, mbili za mwezi wa saba na nane na moja mwezi wa tisa, hata ukikaa mwaka bila kununua siku ukinunua unakatwa buku 12
 
Leo ni mwezi wa ngani na mwisho ulinunua mwezi lini ?

In short mpaka leo inabidi uwe ushakatwa buku 3, mbili za mwezi wa saba na nane na moja mwezi wa tisa..., ukikaa miaka mwaka bila kununua siku ukinunua unakatwa buku 12
Asante kwa ufafanuzi mkuu sikuyajua haya kabisa

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Leo ni mwezi wa ngani na mwisho ulinunua mwezi lini?

In short mpaka leo inabidi uwe ushakatwa buku 3, mbili za mwezi wa saba na nane na moja mwezi wa tisa, ukikaa miaka mwaka bila kununua siku ukinunua unakatwa buku 12

Tozo juu ya tozo katikati ya janga la Corona kwa hakika ni Tanzania tu.

Sawa na wasimamishe uchumi wao kwanza.
 
Leo ni mwezi wa ngani na mwisho ulinunua mwezi lini?

In short mpaka leo inabidi uwe ushakatwa buku 3, mbili za mwezi wa saba na nane na moja mwezi wa tisa, ukikaa miaka mwaka bila kununua siku ukinunua unakatwa buku 12
Hii hatari sana halafu wanaandika debt, ajabu pamoja na kulipa hilo tozo kwa njia za kawaida na tozo ya mwaka 10,000 bado wanakata kwenye muamala.
 
Wakuu habari za jioni kwa mashabiki wa biashara United timu Bado haijatoka hadi mda huu kwenda Djibouti.

Niende kwenye mada kuu naomba kuuliza wakuu mnisaidie juu hili tuliambiwa kodi hii itakuwa inakatwa kila mwezi lakn maajabu Leo nimenunua umeme naona inakatwa tena hii kodi

Au n Mimi sikuelewa tangazo lao au wameamua kujichukulia sheria zao binafsi

Wakumbuke wengne umeme tunanunua wa 1000 kulingana na vipato vyetu sasa naona wanatulazimisha kinyume na makubaliano tuliyo kubaliana hapo awali

Kwa wanasheria siwezi kuwashtaki hawa Tanesco na wizara ya ardhi naona kama wamevunja makubaliano

Cc TANESCO @Petro E. Mselewa @Pascal Mayalla

Sent from my TECNO F1 using [URL='http://r.tapatalk.com/byo?rid=77694']JamiiForums mobile app[/URL]
TAFADHALI onyesha namba ya mita tukujibu kwa taarifa kamili kwa kuwa hakuna mabadiliko yeyote yale isipokuwa mteja anakatwa mara moja kwa kila mwezi atakaonunua umeme
 
Wanakata kwa mwezi mara moja mfano; Mwezi wa nane na wa tisa jumla 2000/= ikifika mwezi wa tisa utalipia tena wa kumi na kumi na moja
 
Hakuna mpangilio maalum ni kodi tu hakuna kitu kingine cha maana , na tanesco walivyo mabingwa wa kuiba hata zile token zilitotakiwa warudishe kipindi kile cha sakata la LUKU hadi leo hawajarudisha, kiufupi ni shida tu
 
Acha kupotosha badala yake toa taarifa kamili za tatizo gani lini na namba ya simu nasisi tupo kukuhudumia
 
TAFADHALI onyesha namba ya mita tukujibu kwa taarifa kamili kwa kuwa hakuna mabadiliko yeyote yale isipokuwa mteja anakatwa mara moja kwa kila mwezi atakaonunua umeme
5418 3826 368

Nimelipa Tsh 4,000/= muda huu halafu nimepata umeme wa Tsh 1,000/=.
Maana yake Tsh 3,000/= haipo
Mwezi uliopita nilikatwa Tsh 2,000/=, sasa naomba unifafanulie lipi ni kosa langu
 
Back
Top Bottom