The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Serikali imependekeza vyanzo vya ziada vya mapato kupitia Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2026/2027 ili kugharamia Mfuko wa Bima ya Afya kwa Wote. Hatua hii itahusisha marekebisho ya sheria yatakayoongeza kodi na tozo kwenye bidhaa za sigara na sukari nchini.
Mabadiliko yaliyopendekezwa ni kama ifuatavyo:
Sigara: Ushuru wa bidhaa utaongezeka kwa Shilingi 20 kwa kila sigara 1,000 zinazozalishwa au kuingizwa nchini.
Sukari: Tozo ya Shilingi 10 itawekwa kwenye kila kilo moja ya sukari inayozalishwa ndani au inayoagizwa kutoka nje, ambapo makusanyo yake yatawasilishwa moja kwa moja kwenye Mfuko wa Bima ya Afya.
Hatua hizi zinatarajiwa kuongeza jumla ya Shilingi bilioni 7.5 zitakazotumika kuimarisha na kufanikisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi wote.
Pia soma: Gharama ya Bima ya Afya kwa wote ni Tsh. 150, 000 kwa kaya, wasio na uwezo kugharamiwa na serikali