Fantastic Beast
Member
- Feb 18, 2019
- 53
- 539
Haya ni maoni yangu juu ya hii tozo ya uzalendo (Ingawaje hili jina limekaa fyongo sana, kwa nini unitoze kwa sababu mimi ni mzalendo?):
- Serikali hasa wizara husika inapaswa kuweka benchmark/fixed rate ambayo kila mzalendo atakatwa kiwango sawa bila kujali kiwango cha muamala anaofanya. Uzalendo ni uzalendo, sote tunapaswa kukatwa kiwango sawa bila kujali ukubwa wa muamala anaofanya mtu. Kitu ambacho hamkijui ni kwamba mkiweka fixed amount ambayo ni affordable kwa kila mtu basi miamala itakuwa mingi na mtakusanya kiwango kikubwa tofauti na sasa. Kwa sasa mnachoambulia ni ile miamala ya dharura ambayo mtu anakuwa hana namna sababu amebanwa.
- Haiwezekani mtu anatuma 1000,000/=, gharama za muamala ni lets say ni 3500/= halafu tozo ya uzalendo ni 8000/=. Hii haijakaa sawa na itafanya watu waache kufanya miamala na mtakosa vyote kodi na tozo. Kwa hizo gharama ni bora nitume hizo pesa kama percel tuu kwa njia zingine kama hamna dharura.
- Serikali inatakiwa ituambie wananchi hii tozo itaenda kwa muda gani, miezi, mwaka, miaka ama muongo kabisa. Sababu ya hizi tozo mmetuambia ni za kujenga barabara za vijijini na vituo vya afya. Lakini hamjatuambia gharama za kujenga hizo barabara na vituo ni kiasi gani, tunapaswa kujua ili hayo makusanyo ya makato yakitimia kiasi kinachotakiwa kwa hizo shughuli basi msitishe makato. Kunatakiwa kuwe na cut-off limit ya muda wa makusanyo pamoja kiasi cha makusanyo sababu "uhitaji" wa hizo huduma utaendelea kuwepo milele na milele sababu kila siku watu wanaendelea kuzaliana na uhitaji utaendelea kuwepo tuu.
- La mwisho kabisa kwa kuwa mmetuambia hii tozo ni ya uzalendo na uzalendo si kulazimishana basi napendekeza iwe ni hiari ya mtu kuchangia ama kutokuchangia. Pia mchangiaji apewe uhuru wa kuchangia kile anachoweza ku-afford sio serikali kuweka rates inazotaka yenyewe.
Tofauti na hapo basi serikali itegemee kuona namba ya miamala ikipungua siku hadi siku.