Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,561
- 24,428
Kwa kweli tozo za utoaji wa fedha kwa mitandao kwa sasa sio rafiki tena kwa Mtanzania wa kawaida ni kummaliza kwani unapotumiwa kiasi cha 10 000 kampuni wanakata kiasi cha shilingi 1000 hii ikimaanisha ni 10% ambayo kwa kweli ni kiwango kikubwa mno na pia ni kama wizi au kumuibia mnyonge ambaye anamtumia mama yake kule kijijini hela ya mbegu washushe viwango vyao hadi kufikia 5% tu kama kweli wanataka kuwasaidia wanyonge wa taifa hili na ndio umaana halisi wa teknolojia za namna hii ni ili ziwe msaada kwa wanaulimwengu.