Chiblak
JF-Expert Member
- Jul 3, 2014
- 662
- 921
Habari wanajamvi poleni na majukumu ya kila siku. Moja kwa moja twende kwenye mada yetu.
Aisee kumekua na hili suala la kutozana tozo mbalimbali ambazo baadhi zimekua sahihi na nyingine si sahihi. Kumekua na tozo ya takataka (sahihi) na pia tozo ya ulinzi shirikishi (si sahihi).
Tozo ya takataka, hii kwangu naona ni sahihi japo na yenyewe ina mapungufu kadhaa. Kawaida tunalipishwa 2000 mpaka 3000 kwa kila kaya kitu ambacho si sahihi kwani kila kaya inazalisha taka kwa kiwango tofauti. Kwa mfano kuna mabachelor wasioshinda nyumbani kabisa na wengine hurudi nyumbani kwa aijli ya kulala tu, kwangu si sahihi kuwatoza kiwango sawa na kaya ya Mama Ally yenye wanafamilia sita.. Badala yake kungekua na mfumo wa kutoza kwa nyumba ili wakazi wa nyumba husika wapangiane wenyewe viwango vya kutozana. Mbaya zaidi watozaji hawatoi risit.
Tozo ya ulinzi shirikishi, hii kwangu ndio si sahihi kabisa kwani tunatozwa 2000 mpaka 3000 kwa kila kaya ila bado watu wanaibiwa na kujeruhiwa kila kukicha. Mimi Nina swali la kuhoji hapa.... Hawa shirikishi tunaowalipa si ni kwa aijli ya ulinzi na usalama wetu na mali zetu? Sasa inamaana inapotokea watu kuibiwa na kujeruhiwa tuna haki ya kuwa hold responsible Hawa watu?Je na wao wanao wajibu ku refund upotevu wa mali na majeraha ya watu? Na Je jeshi letu la polisi Lina majukumu gani ikiwa shirikishi wasio na mafunzo yoyote ya kijeshi wanapewa jukumu la kumlinda raia mwenzake? Mwisho shirikishi wamewekwa kwa mujibu wa sheria ni Nani mwenye wajibu wa kuwalipa?
Mwisho .... Hizi tozo hupangwa huko serikali za mitaa pasipo hata sisi wana mtaa kushirikishwa!.. kumalizia hata Kama tutashirikishwa na kukubaliana basi tuzingatie utoaji wa risit za EFD.