Tozo za Miamala: Tunaelekea kuzungumza lugha moja

Tozo za Miamala: Tunaelekea kuzungumza lugha moja

Ss Jr

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2018
Posts
577
Reaction score
451
Ongezeko la tozo za Serikali kwenye miamala ya fedha zimekuwa gumzo kila kona na kuanza kuondoa matumaini kwa Watanzania wa kipato cha chini ambao wamekuwa wakiitumia mitandao ya simu kama vibubu vya kutunza fedha kidogo kidogo na kutuma na kutumiwa fedha hata kwa watoto walioko mashuleni.

Ukipita kila kona kwa kiwango kikubwa watu hawana hamu ya kuendelea kutumia miamala ya fedha kwenye mitandao ya simu, hata wapambe wa Mama wako kimya wasijue la kufanya wanaogopa kuhojiwa maana furaha yao imegeuka kuwa huzuni,Ni ukweli usiopingika tunakoelekea tutazungumza lugha moja.View attachment 1855538View attachment 1855539
IMG-20210715-WA0000.jpg
 
Tutulie tu dawa ituingie.
Hii dawa ni yetu sote sasa wazee wa mboga mboga nao wanalalamika mitaani huku
Screenshot_2021-07-16-07-54-34-58.jpg
 
Ni matokeo ya ccm kubaki madarakani tangu uhuru.
 
Ila acha watu wanyooshww
Nchi iliendeshwa kwa kodi za watu wachache tu kubeba mzigo wa wengi

safari hii kila mtu imoooo
 
Kwa Moyo wa dhati kabisa niwapongeze wanywa Bia na Wavuta Sigara popote pale walipo..
Wamelipa Kodi miaka yote kwa Uzalendo mkubwa bila malalamiko na Nchi ikafikia Uchumi wa Kati.
Serikali ikaona iwapunguzie kidogo kwenye local beers Kama Bakshishi,na ikatengeneza Kodi ya Kizalendo....
Wanywa Chai, Soda Na Juice Sasa, Nchi Haikaliki... Malalamiko kibao..

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
FCC Hawahusiki hapa?...Au Kamanda Siro hana nafasi...! Nani Aokoe Jahazi..! BASATA au TCRA hawana Uwezo aidha wawafungie ama Wawazimie Mitambo...Hii ni too Much
 
Hivi kesho namba moja akirudi akasema tunabidi hii ni kodi wanatafuta ela ya chanjo ya Covid nina uhakika kuna watu waliokengeuka leo watakuja kuitetea hii hii kodi🤣🤣
 
Back
Top Bottom