Tozo za miamala zimekuwa kero kwa wananchi, serikali imeshupaza shingo

Tozo za miamala zimekuwa kero kwa wananchi, serikali imeshupaza shingo

RWANDES

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,788
Reaction score
4,401
Ni kilio cha kusaga meno kila kona ya nchi tozo imekuwa mwiba mkubwa kwa wananchi kila kona wanalia hata hivyo baadhi ya wafanyakazi wa umma hasa manesi na walimu wanalalamika sana kuona wanalipa kodi huku tena kuendelea kukatwa fedha zao zaidi ya maratatu kupitia tozo ambazo imeweka serikali kupitia mishahara yao.

Kwa sasa serikali haina ubunifu wa vyanzo vya mapato inapambana na wanachi ikumbukwe kuwa siyo tozo tu hizi ambazo kwa sasa imeamuwa kuziweka bali angalieni nyie wenyewe mfumuko wa bei za bidhaa siyo mafta siyo nondo siyo bati siyo vyakula kila kitu kimepanda bei na fedha hamna! serikali ya awamu ya sita utetezi wake kwa kika kitu ni vita ya Urus & Ukraine kama siyo vita ni ugonjwa wa uviko19 naona mama anachokitafta atakipata soon ataona rangi halisi za wananchi.

Kwa sasa hakuna unafuu wa maisha na waliiwengi humu ambao ni walamba asali wanakuja na majibu ya fanya kazi acha kulalamika nani hafanyi kazi kama hufanyi kazi unaweza kuja kuweka hoja humu, ndugu zangu situkeni mambo yamekuwa magumu ni wakati wakuamua juu ya nchi yetu! hii nchi siyo mali ya kikundi cha watu ni mali ya watanzania wote. atakumbukwa kwa ujumbe mzuri kabisa msaani huyu[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

 
Ukiwauliza utasikia tozo zinatumika kujenga hospital na shule. Me naomba uwaulize kikwete serikali yake ilisifika kwa kulipa mishahara hewa na ufisadi.

Ila serikali yake ilifanikiwa kuanzisha na kujenga shule za kata, kuipa nguvu sekta ya afya na elimu.
 
Ubunifu utatoka wapi kama watu wenye mamlaka hawana ubunifu wowote ule wenye tija vichwani mwao!
Walio kuwa wana wapa mawazo mbadala waliwatoa bungeni. Bunge lime baki kusema ndiyo kila kitu.

Mamilioni ya pesa wana lipwa wabunge hewa walio chongwa. Bado serikali haioni soni.

Ina walinda kwa gharama kubwa za walala hoi.

Tuna minywa kwa tozo ili wao wapande V8.

Unaijua V8 wewe?
 
Mkivaa nguo za kijani huwa mnajitoa ufaham kwa kauli za "kidumu Cha Cha fisiemu" ,"Tunatetea chama" nk Sasa huu ndo muda wa kula matunda ya kutetea chama na kidumu chama tawala
 
Vyema selikal ikaangalia vyanzo vingine hii kuumiza wananchi
Kodi ni nyingi.

Mwigulu ni msomi wa uchumi
Tunaomba elimu yake ikomboe taifa
Makato ni mengi mno.
 
Leo watu wengi wanalialia hela zao zimefwekwa huko NMB.

Mimi sitaki kuamini Kama ni kweli ila siwapuuzi wote wanaolialia hela zao kukatwa,
maana Mimi sijakatwa sababu kamshahara kangu kakiingiaga tu nikipata notification muda huohuo naenda kutoa hela zote ikibaki hela chini ya elfu kumi napita kwa wakala kuimalizia yaana nahakiki hamna kitu kilichobaki.
 
Mkuu utakuwa ulikuwa na transactions za B na ushee
 
Vyema selikal ikaangalia vyanzo vingine hii kuumiza wananchi
Kodi ni nyingi
Mwigulu ni msomi wa uchumi
Tunaomba elimu yake ikomboe taifa
Makato ni mengi mno
Huwa wanakarjri tu hawaelewi. Watu wanapata PhD faster tu!
 
Back
Top Bottom