Tozo za simu: Bunge limeaibika!

Kwenye ngazi ya urais sio rahisi ki hivyo kwani yeye hata asipopata kura nyingi , bali tume ya uchaguzi tu ikishamtangaza tu kuwa ndio mshindi biashara imekwisha, hakuna pa kwenda, lakini kwenye ubunge mtu anaweza kwenda mahakamani na ubunge ukatenguliwa!!au akavunja bunge yeye uhakika wa kurudi ni 100% wabunge hao wote wakapigwa chini kwenye kura za maoni akaweka wapya na ukafanyika umafia kama 2020!!akawa amewakomoa!!siasa za nchi za kiafrika unazijua wewe?!!
 
Pumba tupu!

Unaongea hisia bila kuangalia sheria
 
Kama nchi kwa kweli tulijikwaa kukabizi nchi na bunge kwa watu wenye mafaili yao milembe.
 
Ni ulaghai kuwataka kuwaaminisha wananchi kuwa tozo zitawapatia huduma za jamii. Ikumbukwe kuwa kodi lukukii, mikopo na misaada kibao kwa miongo kadhaa vimeshindwa kufua dafu
Wameshatuona watz, ni pimbi tu ni miaka mingapi wamekuwa wakituaminisha kuwa wanapunguza kodi kwenye gesi ili kila mtanzania atumie gesi kupikia ili kuachana na mkaa, na kipindi wanapigia chapuo mradi wa gesi asilia wa Mtwara, kuwa ni neema kwa Watz, hadi leo nini kimetokea?!!nchi hii hakuna kiongozi mwenye uchungu na wanyonge, jitu linakwambia eti tozo hizo zitatumika kujenga vituo vya afya 900!!leo tu panadol kwenye hospital ni tabu!!eti maboma ya shule 1000!!hao watoto leo hawana madawati!!hakuna lolote na hizo pesa wanahangaika nazo ni za kumalizia hayo ma miradi waliyoyaanzisha kwa kutafuta sifa tu, na sio kitu kingine!!WANA MHAHO!!kwani mambo mengi ya muhimu yalisimama , mfano ajira, nyongeza ya mishahara, kulipa madeni ya wazabuni, sasa Mama, amejitahidi kuyafungua, kushituka huku, pesa ndio hivyo tena, anafanyaje?!
 
Pumba tupu!

Unaongea hisia bila kuangalia sheria
Wewe ndio hujui kitu yaani kwa akili zako kabisa Rais wa TZ, anaweza kuhofia uchaguzi kuwa eti akilivunja bunge anaweza asirudi madarakani?kwa katiba hii ?!!sheria ipi unayoizungumzia wewe?!!bunge ambalo halina mizizi yoyote limeelea tu juu , juu, litakuwa ni bunge?hapa kuna bunge au ni kamati ya chama tu?!!
 
Kwa katiba hii iliyopo Rais atarudi akiwa pamoja na matakataka yote ayatakayo kwa maslahi yake.
TUME ya uchaguzi, yake. Wasimamizi ni ma DED wake. Ma Polisi ni walewale akina Siro na Kakwale. TISS wanaotetea maslahi ya CCM
 
Ha ha ha ha haaaaaaaaa bunge la ccm hilo,"WAPINZANI WALICHELEWESHA SANA MAENDELEO,KILA KITU KUPINGA" By Magufuri the hero of ccm.
 
FACT.
 
Hatuna haja ya kuwa na bunge kama tunaweza kuisimamia, kuishauri na kuiwajibisha serikali sisi wananchi wenyewe. Naona wabunge wapo upande wa serikali. Sioni umuhimu wao tuseme tu ukweli
Suala la kifurushi bunge letu lilikuwa kimya.

Suala la tozo za miamala bunge letu liko kimya.

Suala la kodi kwenye pembejeo bunge letu liko kimya.

Suala la kodi kwenye mafuta bunge letu liko kimya.

Halafu bado tunaliita bunge, wananchi tunakila sababu za kujisemea sisi wenyewe tu.
 
Aibu kubwa sana kwa Spika, baraza la mawaziri, wabunge kwa ujumla wao na kamati ya bunge ya bajeti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…