KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Habari za wakati huu.
Mimi ni mkazi wa Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, na ni Mfanyabiashara wa hapa mjini Bariadi ambako ni makao makuu ya Mkoa wa Simiyu, lakini makazi yangu yapo hapa hapa Mjini.
Hivi Karibuni uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ulileta mzabuni mpya wa kukusanya taka kwenye Halmashauri yetu.
Mzabuni huyu kwa sasa ana kama zaidi ya miezi mitatu, jambo la ajabu na kusikitisha maana hatuelewi, Je? Gharama za kukusanya taka ni Sh. Ngapi?
Huyu Mzabuni kuna sehemu kwenye maduka yetu, anakuja anadai mtu ulipe Sh. 10,000 kwa mwezi, maduka mengine Sh 5,000, kwingine ni Sh. 2,000.
Tunaomba uongozi wa Halmashauri utwambie Sheria ndogo imeweka tozo kiasi gani tunayotakiwa kutozwa sisi Wafanyabiashara kwa ajili ya uchafu na hata kwenye makazi ya watu?
Huu mkanganyiko, tunauona ni kama wizi mkubwa unaofanywa na wakusanyaji, kwanini kiwango kisieleweke? Na kwa nini hakiko wazi?
Tunaomba kuelezwa na ikiwezekana hizi tozo zibandikwe kwenye mbao za matangazo ili kila Mmoja afahamu ni kiasi gani anatakiwa kutoa.
Kwa jinsi tunavyojua, kiwango cha tozo za uchafu hakizidi Sh. 5,000 kwenye vibanda au maduka ya biashara, lakini kwa makazi ya Watu hazidi Sh. 1,000 au Sh. 2,000.
Sasa hizi tozo za hadi Sh. 10,000 zinatoka wapi? Huu ni wizi, tunaomba ufafanuzi kama tunaibiwa au hapana, na kama tunaibiwa tunaomba turejeshewe pesa zetu ambao tumetozwa.