Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa Jijini Dodoma leo ameshiriki hafla ya utiaji saini mikataba ya miradi ya kufikisha huduma za mawasiliano ya simu katika Kata 763 nchini na miongoni mwa aliyoyasema ni kuhusu Watoa huduma za mitandao ya simu kudai tozo wanazowekewa ni kubwa hasa kwenye mamlaka za Serikali na Hifadhi mbalimbali na kwamba tozo hizo sasa ndizo zinafanya hata mabando yao kuwa ya bei juu.
Rais Samia amesema “Tozo moja waliyoilalamikia ni ile ambayo Mh.Spika ameizungumza tozo ya kupitisha mkongo kwenye eneo la akiba ya barabara”
“Kuna Taasisi kadhaa zinatumia maeneo yale tozo zipo chini lakini mkongo ni dola Elfu 1 kupitisha kwenye maeneo yale, sasa hiyo haiwi bure wanakwenda kutuongezea gharama ya bando, lazima Serikali tuliangalie hili ili kushusha gharama”