Klabu ya TP Mazembe baada ya kutoka sare na CR Belouizdad ya Algeria, mchezo uliopigwa nchini DRC, TP Mazembe imeendelea na kukubwa na mzimu wa sare ya pili mfululizo baada ya Jana February 24, 2021 kulazimishwa sare ya kutofungana na Al Hilal SC ya Sudan katika michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika.
Kwa sasa ni dhahir kuwa mpira umebadilika sana na kila zama na watu wake, ubora umepungua kwa Klabu ya TP Mazembe kwa msimu huu tofauti na miaka iliyopita kwasababu walikuwa na uwezo wa kushindana na kupambana mpaka ushindi hatimaye kushinda ubingwa.
Mechi...2
Ushindi...0
alama..2
Kupoteza..0
Goli...0
Msimamo wa kundi B klabu bingwa Afrika.
1. Mamelodi> mechi 1 alama 3
2. TP Mazembe> mechi 2 alama 2
3. CD Belouizdad> mechi 1 alama 1
4. Al Hilal Omdurman> mechi 2 alama 1
Kwa sasa maji yamekorogeka TP Mazembe na inashtua kuona sare ya pili mfululizo na huenda likawa daraja la Simba SC kuvuka hatua ya robo fainali na kutinga nusu, endapo watakutana kwenye hatua ya robo fainali.