Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata mabonanza yana kombe.....mkuu 😀 😀Hakunaga kombe la siku mbili mkuu....lile ni bonanza
Nakukubari chambuzi la kimataifa“Tumepokea ugeni mzito kutoka moja ya Klabu kubwa Barani Afrika, TP Mazembe ya DR Congo ambao wamevutiwa na namna Klabu yetu ya Yanga inavyoendeshwa hivyo wamekuja hapa Tanzania kujifunza mambo mbalimbali kwenye Mfumo wetu wa Mabadiliko ya Uendeshaji" Simon Patrick, Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga SC.
---
Pia tutakuwa na makubaliano rasmi ya urafiki wa kushirikiana kati ya Klabu yetu ya Yanga na TP Mazembe ili kuweza kubadilisha ujuzi wa mambo mbalimbali ya kimpira yatakayoweza kuisaidia Klabu yetu.
Klabu kubwa kama TP Mazembe imesafiri kutoka DR Congo kuja hapa Jangwani kujifunza kwa kichwa chetu, Rais wetu Eng. Hersi Said halafu kuna watu wako nyumba ya 16 tu jirani hapo, wanapiga kelele kuwa hawana cha kujifunza kwa Yanga. Niwaambie tu, tutabeba Makombe hadi kila Mwanachama atakuwa anabeba la kuweka nyumbani kwake
#timuyawananchi
#daimambelenyumamwiko
Je Kuna ukweli kuwa Yanga ndio workshop ya soka hapa Afrika???
Uzuri Yanga anapohitaji kujifunza anakuwa mnyenyekevu sana tofauti na wale jamaa wanaoamini na wao ni wakubwa wanajiweka level moja na Al Ahly, Esperance, Zamaleki na wengine hivyo hawana cha kujifunza.Yanga nao watumie muda huu kujofunza toka kwa Mazembe
Wao Mazembe wameona kuna cha kujifunza Yanga, Wewe Mbumbumbu unasema hakuna.TANZANIA KUNA WAJINGA WENGI SANA .SASA MAZEMBE ATAJIFUNZA NINI KWA YANGA.??? AU KUJIFUNZA KUHONGA MAREFA.??? MANA YANGA KAZIDIWA KILA KITU NA MAZEMBE
Wakati huo fungu la gharama za uendeshaji wa timu linatoka wapi?Mo hakuna anachomiliki pale ni mpigaji tu.kwemye dili la jezi ya 40,0000.utopolo anachukua 1,300.sio upigaji huo?ndo maaana nakwambia utopolo kumetulia sababu kumepona ugonjwa ila ukianza up ya tutajua mengi.
Mazembe bado hajarudi kwenye ubora wake. Kwenye ubora wake huwa anachukua makombe. Usumbufu wanao kina Mwakarobo.Hivi unavyoviita success ni kituko, ukisema hivyo unataka kusema Simba Sc kuchukua PL trophies 4, FA Cups 4, CAFCL & CAFCC quarter finals mara 3 (wakati huo) yaliluwa ni majibu ya uwekezaji?
Kwahiyo Simba Sc nayo ungesimama kutamba? Sioni inachofanya Yanga Sc au kombe ililobeba Yanga Sc ambalo Simba Sc hijawahi, kilichopo ni swala la kupokezana mafanikio kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Mazembe hana cha kujifunza kinachohusu mpira kwa team za Kariakoo. Maana wao hata baada ya kuanguka, iliwachukua mwaka mmoja tu (msimu uliopita) kujipanga na sasa wamerudi kuwa wasumbufu kwenye soka la kimataifa.
Kama hawakuelewa na hapa sina budi kuungana na Aden Rage.Football club nyingi za Africa zinazomilikiwa na mtu binafsi zina matumizi mabaya ya pesa. Hali hiyo hupelekea kuyumba kwa mmiliki wa timu na kuamua kuitelekeza kama ambavyo Mo amefanya mara kdhaa na baadae hurudi kwa mapenzi yake. Timu nyingi hazijiendeshi kitaasisi kiasi kwamba mmiliki akipitia changamoto na timu inakuwa kwenye changamoto kama ilivyokuwa kwa Moses Katumbi na Mazembe.
Yanga imepitia hali hizo pia. Mfadhili alipopitia misukosuko na timu ilipitia wakati mgumu sana mpaka alipopatikana GSM. Jambo zuri GSM alipata ushauri mzuri mapema wa namna ya kuzitumia pesa zake . Lakini wazo kuu likawa kufanya transformation wa namna ya kuendesha timu tofauti na utaratibu wa kijima uliozoeleka ambao haukuwa na faida kwa zaidi ya kuifanya kuwa ombaomba.
Kwenye eneo la kiuongozi Yanga imefanikiwa sana kuwa transformed. Na matokeo ya transformation hiyo ya uongozi yameonekana uwanjani hata kama timu haijachukua kombe.
Kunapokuwa na matokeo mazuri uwanjani lazima yataonekana tu. Kupitia mafanikio hayo imekuwa rahisi kwa Rais wa Yanga kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa vilabu baroni Africa. Mnafikiri imekuja kwa bahati tu? Hapana. Kuna jambo limefanyika. Iliwahi tokea wakati Simba ikifanya vizuri CEO wake Babra aliteuliwa kuwa mmoja wa wanakamati za CAF.
Mazembe wanahitaji transformation ya kuendesha timu kutoka kwenye kutegemea maamuzi ya mtu mmoja na kuwa na proper structure ya uongozi. Na hii itaisaidia Tp Mazembe kwa miaka mingi. Mazembe hawana mashabiki waliowasajiri kidigitali na kama wapo ni kwa idadi ndogo sana na hili wanalipitia pia Mamelodi, hili pia wanaweza kujifunza kutoka kwa Yanga kwa kuwa ndio timu iliyofanikiwa kwenye kipengele hicho kwa ukanda huu hata kama sio kwa kiwango kikubwa lakini mapato yanaonekana.
Mambo ni mengi ambayo Tp Mazembe wanaweza kudesa toka kwa Yanga ili waweze kujiendesha hapo baadae Moses Katumbi atakapokuwa hayupo. Na huenda desa hili likawanufaisha zaidi Mazembe kuliko Yanga yenyewe.
Mazembe ni kubwa kimafanikio kuliko Yanga kimataifa na kipesa huenda. Lakini hatuna uhakika kama ikitokea sheria ya Financial fair play ikaja Africa kama Mazembe, Yanga na timu nyingine zitaweza kujiendesha. Ndio maana kunahitajika Transformation mapema sana.
Inasemekana Nigeria walichukua desa la makao makau yao kutoka ramani ya Dodoma na haimaanishi Tanzania ilikuwa imefanikiwa kuliko Nigeria
Usikute wewe ni Mangungu unajaribu kuyahadaa Makolo yaamini mafanikio ya Wananchi yametokana na kuhonga marefa.Wanafundishwa jinsi ya kutuma miamala kwa marefa