TPA wamepokea tuzo kwa kuwa shirika bora Tanzania, jamani ni aibu kulete DP kwa kweli

Maandalizi ya kuitema dpw yanaweza kuanza!!! Na dpw watashitaki kwa usumbufu watalipwa na hela baadhi zitatumika Kurudisha watu kwenye nafasi zao za uongozi muda si mwingi! Tunachezewa sana!!!
 
Nimeshangazwa zaidi ati hata NIDA wamejizolea zawadi

Au kuna NIDA mbili hapa Nchini yaani bila jiwe mbili hujapata kitambulisho au nacho ni kiwanda cha mapato ya CCM?

Nimesikitika sana leo mpaka nimeizima luninga
 

Tuzo imetolewa na nani ndo issue, issue sio tuzo, mke wangu ananipa tuzo kila siku, sasa shida tuzo nani ameitoa?
 
Kwahiyo suala la ufanisi mbovu siyo hoja tena ?
 
Hapana, siyo kwa kuwa ni shirika bora. Usiseme uongo.

Wamepewa tuzo kwa kutowa pesa serikalini kwa mara ya kwanza baada ya kufanyiwa reforms. Tena wao ni wa pili kati ya mashirika matano yaliyotambuliwa mchango wao. La kwanza ni Twiga Cement.

Tena ni pesa ndogo sana ukilinganisha na uwekezaji uliofanyika bandarini.
 
Ndo tujue kuna wenzetu wameamua kutupiga mnada makusudi. Ndugai hakukosea kipindi kile.
 
Ukiwa muongo unatakiwa kuwa smart.
 
Kuwa wa kwanza haimaanishi kuna ufanisi. Kwa taarifa yako NIDA kashika no 3! Hali ya NIDA ikoje?
 
Kuwa wa kwanza haimaanishi kuna ufanisi. Kwa taarifa yako NIDA kashika no 3! Hali ya NIDA ikoje?
Ngonja nikuambie kitu ,ufanisi ni kitu endelevu.TPA wanaendelea vizuri na muda baada ya muda wanaongeza ufanisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…