TPA yahamishia shughuli zake Dodoma

TPA yahamishia shughuli zake Dodoma

mirindimo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
901
Reaction score
1,742
12A42228-3B51-4CDD-99F9-598B43D70555.jpeg
 
Huku ulipotaja at least kuna shughuli za majini hivyo ofisi ni muhimu.. hapo Dodoma wanaenda kuhudumia bwawa la Mtera??
Soma Tangazo Tambua katika kila bandari zote ,dar ,Tanga, mtwara, mwanza, kigoma, Nyasa, bukoba Kuna ofisi zao sasa hapo dar itabaki kama regional office makao makuu yatabaki kuwa Dodoma na zile operation za dar zitakuwa vile vile kama kawaida huko HQ Dodoma patakuwa na ishu za watu wa juu tu katika mamlaka
 
Kilichoagizwa na Magufuli kitabaki vilevile nyumbu wavimbe na wapasuke
 
Hwajui ilo wakati ukienda bukoba ,Nyasa, mtwara, Tanga, Dar ,mwanza ipo ofisi za TPA za regional operation ila management ilikuwa dar kwa sasa Dodoma hamna tatizo maana kule ni ishu za top management sio subordinates
Operation Vs Magenament
....... Management inaweza kuwa ulaya, Operations zinafanyika Buzwagi!!!
 
Elimu yetu inatukaririsha namna ya kujibu swali Ila Ile real understanding how to tackle that problem in life related haipo.

Mfano mzuri binafsi nimesoma maths Ila baada ya kuingia mtaani ndipo nikaijua Ile probability katika statistics inatumikaje na ndio naishi kwa iyo topic ya hesabu pia hasi na chanya . Ila at that time I was very sensitive how to answer the question nipate maksi zote ujue. Kweli ukimaliza shule ndio unaanza kusoma Sasa kwa vitendo nimeamini na ndio shule halisi muda mwingi mno tunatumia katika dhahania.

Yaani inatosha kijana akatoka chuo akatoka ama like 20yrs halafu 20-25 apate degree ya Pili kwa practical kabisa. Yaani muda wa theory upunguzwe. Mana hizo zipo tu Kama mtu anakwama sehemu theory inayomsadia katika practical atazitafuta azipitie Kama hakuelewa vizuri. Napendekeza msingi iwe 5 kijana atoke akiwa na 10yrs na sekondari iwe jumla minne,atakuwa ana 14 baadaye chuo iwe mitano atoke akiwa 19 ,aingie kitaa Sasa kutumia tricks alizozipata chuoni ama shuleni.

Muda mwingi autumie mtaani na sio shuleni.
Wewe unajua mamlaka ya bandari ina deal na bandari ya Dar tu .vp kigoma,mwanza, bukoba, na nyasa kasome shule tena uache umbumbum usiku

USSR
 
Sisi hata kuiga hatujui.
Kipindi Cha Uhuru Kenyatta shughuli za bandari ya Mombasa zilihamishiwa Naivasha, lkn uongozi wa Sasa ulivyoingia madarakani waliona Hilo kosa na kumrudisha shughuli zote mombasani.
 
Jambo la kushangaza sana, bandari kukimbia toka pwani.

Hizi gharama za kuendesha ofisi, umangimeza n.k zitazidi kuifanya TPA kukosa ufanisi.

Mkurugenzi mkuu alitakiwa abaki pale Dar es Salaam TPA akiwa na ofisi ghorofa ya 30 akiangali je kuna meli ngapi gatini, zimekaa siku ngapi zikupakuwa na kupakia, je yard ya magari ya IT bandarini imejaa? n.k


Sasa huko Dodoma vitu hivyo vyote ataweza mkurugenzi mkuu kuviona 'live' au atatumia Zoom?

Kuwepo mkurugenzi mkuu Dar es Salaam angeweza kutoka ghorofani kwenda yard au gatini kuulizia alichokiona kupitia dirishani akiwa ghorofa ya 30 ofisini kwake kwanini kuna mkwamo wa ufanisi n.k Sasa huko Dodoma atafikaje yard wharf na gatini?


Mtu kutoka Katanga Lubumbashi Congo DR akitaka kuonana na mkurugenzi mkuu wa TPA asafiri kwenda Dodoma?


More about :
Mamlaka ya Bandari Tanzania


VIDEO TOKA MAKTABA:
24 November 2021


MIKAKATI YA TPA KUVUTIA NA KUTOA HUDUMA KWA UFANISI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Erick Hamis amesema wamedhamiria kuondoa kero za kibiashara kati ya wasafirishaji wa mizigo kutoka nchini Congo, lengo likiwa ni kuongeza uwezo wa kulihudumia soko la nchi hiyo.
Source : mwananchi digital
 
Back
Top Bottom