Jambo la kushangaza sana, bandari kukimbia toka pwani.
Hizi gharama za kuendesha ofisi, umangimeza n.k zitazidi kuifanya TPA kukosa ufanisi.
Mkurugenzi mkuu alitakiwa abaki pale Dar es Salaam TPA akiwa na ofisi ghorofa ya 30 akiangali je kuna meli ngapi gatini, zimekaa siku ngapi zikupakuwa na kupakia, je yard ya magari ya IT bandarini imejaa? n.k
Sasa huko Dodoma vitu hivyo vyote ataweza mkurugenzi mkuu kuviona 'live' au atatumia Zoom?
Kuwepo mkurugenzi mkuu Dar es Salaam angeweza kutoka ghorofani kwenda yard au gatini kuulizia alichokiona kupitia dirishani akiwa ghorofa ya 30 ofisini kwake kwanini kuna mkwamo wa ufanisi n.k Sasa huko Dodoma atafikaje yard wharf na gatini?
Mtu kutoka Katanga Lubumbashi Congo DR akitaka kuonana na mkurugenzi mkuu wa TPA asafiri kwenda Dodoma?
More about :
Mamlaka ya Bandari Tanzania
DAR ES SALAAM PORT DOCUMENTARY Dar es Salaam is Tanzania’s principal port that handles about 95% of Tanzania’s international trade. The port serves the landlocked countries of Malawi, Zambia, DR Congo, Burundi, Rwanda and Uganda. According to World Bank analysis, if Dar es Salaam port reached...
VIDEO TOKA MAKTABA:
24 November 2021
MIKAKATI YA TPA KUVUTIA NA KUTOA HUDUMA KWA UFANISI
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Erick Hamis amesema wamedhamiria kuondoa kero za kibiashara kati ya wasafirishaji wa mizigo kutoka nchini Congo, lengo likiwa ni kuongeza uwezo wa kulihudumia soko la nchi hiyo.
Source : mwananchi digital