TPA yapunguza Tozo ya uendelezaji miundombinu kwa asilimia 50

TPA yapunguza Tozo ya uendelezaji miundombinu kwa asilimia 50

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetangaza kupunguza tozo ya Uendelezaji wa Miundombinu Mipya ya Bandari (PID) kutoka asilimia tisa hadi asilimia 4.5 ya kodi ya forodha.

Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa TPA, Dk. George Fasha, amesema uamuzi huo unalenga kuongeza ushindani wa bandari za Tanzania na kutoa nafuu kwa wafanyabiashara pamoja na wadau wa usafirishaji.

Uamuzi huo umetokana na maoni ya wadau wa sekta ya bandari na dhamira ya serikali kuhakikisha biashara zinaendelea katika mazingira rafiki. TPA imefanya maboresho hayo baada ya kupokea maombi kutoka kwa waingizaji na wasafirishaji wa mizigo waliotaka kiwango hicho kipitiwe upya, huku kiwango hicho kipya kikitarajiwa kuanza kutumika rasmi Julai Mosi, mwaka huu.

Tozo hiyo ilianzishwa mahsusi kusaidia upatikanaji wa fedha za ujenzi na upanuzi wa miundombinu ya bandari kutokana na ongezeko kubwa la shehena nchini. Mapato yatakayopatikana yataelekezwa kwenye miradi ya kimkakati yenye thamani ya Sh trilioni 16.1 katika kipindi cha miaka mitano ijayo, ikiwemo ujenzi wa magati mapya Dar es Salaam, upanuzi wa bandari za Tanga na Mtwara, na ujenzi wa bandari mpya ya Kisiwa Mgao.

Kati ya fedha zinazohitajika, Sh trilioni 11.2 zinatarajiwa kupatikana kupitia mapato ya huduma za bandari na sehemu iliyobaki itatoka kwenye ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi (PPP). Uwepo wa chanzo hiki maalumu utawezesha utekelezaji wa miradi kwa wakati na kuongeza uwezo wa Tanzania kuhudumia nchi za Afrika Mashariki na Kati, ambapo shehena inatarajiwa kufikia tani milioni 62 ifikapo mwaka 2030/2031.

Takwimu za TPA zinaonyesha ukuaji mkubwa wa sekta hiyo, ambapo katika miezi tisa ya mwaka wa fedha 2025/2026, bandari zote nchini zilihudumia tani milioni 29.6 za shehena. Aidha, kwa mara ya kwanza katika historia ya sekta hiyo nchini, mamlaka imefanikiwa kuhudumia makasha zaidi ya milioni moja, jambo linaloashiria kuongezeka kwa ufanisi na imani ya wateja


Pia soma: Mamlaka ya Bandari yasogeza mbele kuanza kwa ada ya uendelezaji wa miundombinu bandari hadi Julai 1, 2026
 
Pungezeni tozo kwenye mafuta ili muwapatie wananchi unafuu wa maisha. Lita 1 ya mafuta kwa bei ya 4000+ mnatuua nyinyi wabinafsi mnaotumia mafuta ya bure kwenye ma V8 yenu ya kifahari.
 
Pungezeni tozo kwenye mafuta ili muwapatie wananchi unafuu wa maisha. Lita 1 ya mafuta kwa bei ya 4000+ mnatuua nyinyi wabinafsi mnaotumia mafuta ya bure kwenye ma V8 yenu ya kifahari.
ongeza bidii ya kazi gentleman 🐒
 
Sasa wewe una kazi gani zaidi ya uchawa
Gentleman,
ni vizuri sana kufanya kazi kwa bidii ili hatimae kuondokana na unyonge wa kiuchumi, unaosababisha mihemko nonsense na kulalamika kusiko kwisha kwenye kila kitu 🐒
 
Gentleman,
ni vizuri sana kufanya kazi kwa bidii ili hatimae kuondokana na unyonge wa kiuchumi, unaosababisha mihemko nonsense na kulalamika kusiko kwisha kwenye kila kitu 🐒
Sawa
 
Back
Top Bottom