TPDC kujenga Bomba jipya la gesi Mtwara

TPDC kujenga Bomba jipya la gesi Mtwara

Getrude Mollel

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2022
Posts
270
Reaction score
362
  • Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeanza mchakato wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Ntorya hadi Madimba lenye urefu wa kilomita 35.
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeanza mchakato wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Ntorya hadi Madimba lenye urefu wa kilomita 35.

Mchakato huo umeanza kwa kufanya mkutano wa uhamasishaji kwa wananchi wa kata ya Madimba, Moma, Mbawala na Nanguruwe kuhusu ujenzi wa mradi huo ambao utaanzia kijiji cha Ntorya.

Akizungumza leo Jumatano Oktoba 5, 2022 kwenye mkutano wa hadhara na wananchi hao, mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dustan Kyobya amesema hatua ya awali ya utafiti wa mkuza utakaotumika kupitisha bomba ulishafanyika na kubaini vijiji 12 vitakavyopitiwa na bomba hilo.

Ametaja vijiji hivyo ni Namayakata, Ngorongoro, Mbawala, Mwindi, Nachenjele, Maili kumi, Ding’ida, Likweta, Minyembe, Namidondi na Mendachi.

Amesema hatua inayokwenda kufanyika sasa ni zoezi la uthamini wa mali kwenye mkuza wa bomba wenye upana wa mita 20.

“Lengo la zoezi hili ni kutambua mwendelezo uliofanyika katika ardhi hiyo ikiwemo nyumba, mazao na mali nyingine kubaini thamani yake na kuandaa taratibu za fidia kwa wamiliki,”ameeleza.

Kyobya amewataka wananchi wa maeneo ya yanayopitiwa na mkuza wa bomba kutoa ushirikiano kwa TPDC, wakati watakapopita kwenye maeneo yao katika uthamini.

Meneja wa biashara ya gesi TPDC, Emmanuel Gilbert amesema utekelezaji wa mradi huo unalenga kuongeza uzalishaji wa nishati ya gesi asilia kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya gesi katika uzalishaji wa umeme, kwenye magari, viwandani na majumbani.
 
Haha

Hii nchi hatari sana, moja alijaisha wamerukia mradi mwingine.
 
Selikari ya Samia vichekesho kweli, juzi Kinana kasema wanajenga barabara njia mbili kutoka Kibaa mpaka Tunduma 😁😂😂Sijajua mchakato imefika wapi! baada ya Magufuli kuondoka akuna mtu mwenye uthubutu anayeweza kuanzisha mradi mkubwa,watabakiza maneno tu,tutajenga Serikali hiko kwenye mchakato hayo tu, Kiongozi mwenyewe nimtu wa bata tu.Ngoja nione niko hapo 👉👉ninasubiri hiyo miradi
 
Isije ikawa usanii mwingine wa kutakatisha pesa kifisadi kama miaka ya awamu ya 4
 
Back
Top Bottom