TPDF ilipozima jaribio la mapinduzi Seychelles

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
Kwa miaka mingi suala hili lilikuwa ni SIRI.

Lakini ktk zama hizi za utawandawazi habari hizi zimeanza kujitokeza.

Kuna makala iliandikwa na Makwaia Kuhenga kuzungumzia tukio hili.

Jenerali Ulimwengu, ktk gazeti la raia mwema, amezungumzia ushiriki wa Brigadier.Hassan Ngwilizi ktk operation ya JWTZ Seychelles.

Waziri Membe pia amewahi kuulizwa na vyombo vya habari na alitoa jibu fupi kuhusu kilichotokea.

Kwa mtizamo wangu haya ni mambo ya kihistoria ambayo yanapaswa kuwekwa wazi. Tusipoandika historia yetu wenyewe, wengine watafanya hivyo na hilo lina madhara yake.



cc Moshe Dayan, Nyenyere, Junior Clinton Mr.
 
Last edited by a moderator:
..kuna kipande kingine cha habari hapa kinazungumzia jambo hili.

..pia natafuta taarifa kama JWTZ waliwahi kuwa-deployed Comoro miaka ya 80 na 70.


source:Seychelles firm keen on fishing joint venture with Tanzania - Export.BY
MTAZAMO, Nguruvi3, Echolima, Mag3, Ludovick Mwijage
 
Last edited by a moderator:
Natarajia kutoa historia ya OPERATION MAHE pindi nitakapopata mda mzuri maana nilishiriki ilikuwa 29 Dec 1981.

Nitaelezea kwa kifupi sana.

Mkuu mbna Part 3 ya vita ya Kagera hukuendelea Tena?
 
Katika kuzima jaribio hili la mapinduzi, ndugu zetu Wakenya walikua wameandaliwa na mabeberu kumsapoti rais wa zamani, Mancham aliyekua achukue madaraka tena...it is a very interesting story, na ushujaa wa hali ya juu toka kwa TPDF...kwenye link hapo kuna extract ya maelezo ya Jack; jamaa ambae alikua kamanda wa mercenaries waliodhibitiwa na TPDF.

gonga hapa...
...inspiring the dreams...: We hope the New EAC shall stand...
 
Natarajia kutoa historia ya OPERATION MAHE pindi nitakapopata mda mzuri maana nilishiriki ilikuwa 29 Dec 1981.

Nitaelezea kwa kifupi sana.

Nasubiri sana...once unaandika naomba ni mention ili isinipite km imeahimishiwa jukwaa lingine.Ningependa sana km Jesh lingesaidia wanajeshi kuandika hizi operations na wao ku endorse zianze ingia mitaani, na pengine ktk movies.

Hii itawaenzi sana wanajeshi, kuwapa heshima na fedha.Jeshi tuu liwe na njia ya kubalance ili story iwe kweli, iwe na mafunzo, na pasitokee upotoshaji au hatari kwa jinsi heshi linafanya kazi sasa.
 

wakenya siku zote wanchagua upande mbaya wa historia.
 
Inasikitisha, angalia red hapo chini:

It was said [Argus 27/7/82] that the American CIA were sympathetic and that the American and Kenyan Governments would give instant recognition to the reinstated Seychelles government.
 
Natarajia kutoa historia ya OPERATION MAHE pindi nitakapopata mda mzuri maana nilishiriki ilikuwa 29 Dec 1981.

Nitaelezea kwa kifupi sana.

Hii ilikuwa 2013, na leo ni 2019.
Huko peke yako mTanzania mwenzangu. Hivi ndivyo tulivyo waTanzania wengi, na kimekuwa kilema cha taifa letu.

Tuendelee kusubiri 'kidogo', maanake tunaamini "Haraka haraka haina Baraka" Sisi ni waumini wakubwa wa msemo huo.

Na kama ulitegemea kuhusisha mahojiano yako na Brig. Hasan Ngwlizi, sasa umepata sababu nzuri zaidi ya kuchelewa au kutotoa kabisa andiko lako hilo.

Hivi kuna wakati nasi siku moja tutaondokana na tabia hii kweli?
 
Na unajua, Kenya ndio wanaofaidi matunda hayo. Walimu wameajiriwa huko mashuleni kwa wingi. Hali ni hivyo hivyo na Namibia na hata Afrika ya Kusini.
Silalamiki wala kulaumu, kwa sababu tulitimiza majukumu tuliyodhani ni kwa manufaa ya taifa letu.
 
Habari za siku nyingi wakuu!! Nimepigiwa simu asubuhi hii ya leo na kutaarifiwa kuwa yule Mtemi wa Pointe La Rue keshatutoka katangulia mbele ya haki kwa kweli kifo hicho kimenistua sana ninaposema Pointe La Rue ni jina la uwanja wa ndege wa MAHE huko kwenye visiwa vya Seychells ambako usiku wa Nov,25,1981 wanajeshi wetu nikiwemo mwenyewe Echolima tulitua kwenye uwanja mdogo wa mpira wa shule kwa kutumia ndege yetu DHC-5 Buffalo(Najua sasa hivi ndege hiyo imeshakuwa-Retired from military oprations)Kisa cha safari hiyo ilikuwa kusaidia jahazi lisizame baada ya Mamluki kutoka uliokuwa utawala wa kibaguzi wa afrika kusini kutaka kumuondoa madaraka Rais Rene wa visiwa vya Seychells,Operation hiyo haiwezi kukamilika bila kumtaka Mtemi wa Pointe La Rue Marehemu Brigadier.Hassan Ngwilizi Baada ya kuzima Jaribio hilo mimi na wezangu tulirejea nyumbani Dec,29,1981.
Ni kweli niliahidi kutoa historia yangu ya Operation hiyo lakini kutokana na mambo mbalimbali ya Ki-maisha sikuweza kufanya hivyo lakini kikubwa Namshukuru sana Mungu kwa kutuweka hai mpaka sasa hivi ili kuweza kuyasimlia haya yote kwangu binafsi ni bahati sana maana wengi wetu wamepoteza maisha kutokana na Post traumatic stress disorder (PTSD) na tulio hai inabidi kumshukuru sana Mungu.Kuna msemo wa Kijeshi unasema Mwanajeshi hafi maana hata akifa Matendo yake yanaishi!!!Kwa maana hiyo Matendo na Operation alizozifanya Brigadier.Hassan Ngwilizi huko Msumbiji walipokuwa wanapambana na Renamo na baada huko kwenye Visiwa vya Seychells matendo hayo hayafutiki bali yanaishi hata leo!!!!.
Gamba la Nyoka
JokaKuu
Mdau
Nicholas J Clinton
majeshi 1981
Kudo
 
Mkuu Asante kwa kurejea jamvini. Nchi yetu ina historia kubwa mno lakini haiandikwi na mbaya zaidi mashujaa wenyewe wanapukutika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…