TPDF ilipozima jaribio la mapinduzi Seychelles

TPDF ilipozima jaribio la mapinduzi Seychelles

Loo!!! post hii ndiyo nimeiona leo kweli hata mimi mwenyewe ninasikitika sana!!!Mambo ni mengi sana katika kutafuta rizki ya kila siku!!!
Haya sasa.

Ulikuwa unafukunua nini hadi ukafika huko wakati huu mkuu 'Echolina'!

Uzuri wa JF ndio huu. Hata uchelewe miaka mingapi, habari utaikuta tu, na ukitaka kuchangia kwa wakati wako unajimwaga tu.
 
Kwa miaka mingi suala hili lilikuwa ni SIRI.

Lakini ktk zama hizi za utawandawazi habari hizi zimeanza kujitokeza.

Kuna makala iliandikwa na Makwaia Kuhenga kuzungumzia tukio hili.

Jenerali Ulimwengu, ktk gazeti la raia mwema, amezungumzia ushiriki wa Brigadier.Hassan Ngwilizi ktk operation ya JWTZ Seychelles.

Waziri Membe pia amewahi kuulizwa na vyombo vya habari na alitoa jibu fupi kuhusu kilichotokea.

Kwa mtizamo wangu haya ni mambo ya kihistoria ambayo yanapaswa kuwekwa wazi. Tusipoandika historia yetu wenyewe, wengine watafanya hivyo na hilo lina madhara yake.

cc Moshe Dayan, Nyenyere, Junior Clinton Mr.
Halikufanywa siri, bali labda watu hawakulifuatilia tu. Kuna mtanzania mmoja aliwahi kuwa mtawala wa Seychells kwa muda mfupi wakati wa mapinduzi yale na ilijulikana waziwazi tu. Ni kwa vile Seychells haikuwa high octane story ndiyo maana haikuvuma sana. Hata Nyerere aliwahi kukiri hadharani kabisa kuwa alipeleka jeshi kwenda kumsaidia msoshalisti mwenzake kule Sychells. Ni kutokana na opereshini ile ndiyo maana Seychells ilikuwa na maafisa waandimizi wengi kutoka Tanzania; kwa mfano mwanasheria mkuu wa Seychelles kwa muda mrefu alikuwa ni mtanzania.
 
Umekatisha story mkuu...unaweza kututajia hao watanzania japo kwa uchache??
 
Umekatisha story mkuu...unaweza kututajia hao watanzania japo kwa uchache??
Siwakumbuki majina yao ndugu yangu; ila kulikuwa na wapare/wachaga kadhaa waliokuwa na nafasi za juu sana serikalini. Nadhani Kanali Ngwilizi, kabla hajawa brigedia, alitawala Seychelles kwa siku moja
 
Mh,HISTORIA ni ya muhimu Sana ingawa Watanzania hatuoni umuhimu wa somo Hilo.
 
Watanzania hatupendi kuandika..inabaki historia ya kusimulia kwa mdomo tu
 
Back
Top Bottom