TPDF(wazee wa kazi) waingilia kati, waamua kulitoa Lori lililozama baada ya makampuni binafsi kushindwa

TPDF(wazee wa kazi) waingilia kati, waamua kulitoa Lori lililozama baada ya makampuni binafsi kushindwa

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
MY TAKE: Kamwe JW halijawahi kushindwa vitu vidogo kama hivi, itawachukua masaa machache kyjamilisha hii kazi hapo Kesho. TPDF hoyeeeeee

=======

Jeshi la Wananchi wa Tanzania limetuma timu ya wataalamu kwenda kutoa lori la mizigo ambalo limetumbukia katika Daraja la Mto Wami kwa zaidi ya wiki moja na kushindikana kutolewa .

Kiongozi wa timu hiyo Kapteni Obed Mwakalobo kutoka Kikosi cha Nyumbu amemwambia Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa kwamba kazi ya kutoa lori hilo imeshaanza na wanatarajia ifikapo kesho iwe imekamilika.

Amesema kwa sasa wataalamu hao tayari pamoja na wazamiaji wameshawasili katika eneo lilikotumbukia lori hilo na wameshaanza kuzamia ndani ya maji kuangalia namna ambavyo lori hilo litakavyotolewa.

Kwa upande wake mmiliki wa lori hilo Mwajuma Selemani ameishukuru serikali kwa kutuma wataalamu hao wa jeshi kwenda kusaidia kutoa lori hilo.

Kwandikwa amesema serikali itasimamia zoezi hilo pamoja na kulifanyia maboresho daraja hilo ili liendelee kutumuka hadi hapo mradi wa ujenzi wa daraja jipya katika mto huo utakapokamilika.
 
joto la jiwe,

Sio kushindwa ni vile vitendea kazi tunavyo/wanavyo kwani hata hao raia wangekuwa navyo si wangelitoa tuu?
 
Sio kushindwa ni vile vitendea kazi tunavyo/wanavyo kwani hata hao raia wangekuwa navyo si wangelitoa tuu?
Hahahaha, nashindwa hata kukujibu sijui nianzie wapi?. Unajua maana ya kushindwa kufanya kazi au jambo lolote maana yake ni nini?
 
Hahahaha, nashindwa hata kukujibu sijui nianzie wapi?. Unajua maana ya kushindwa kufanya kazi au jambo lolote maana yake ni nini?
Wee unataka kunipeleka niamini kuwa hilo gari bila jeshi lisingekaa litolewe hapo kabisa. Ni kitu ambacho mimi bado ni ngumu kiniaminisha bado
 
Hivi hata kwa akili ya kawaida hiyo gari yaweza toka kwa kuifunga minyororo na kuivuta
Jeshi wametoa kwa kulisukuma?

Yaani sijui nikutukane mtusi mkubwa wa kwenye chupi yako ndio unielewe au?

Nimesema hivii!!!jeshi wao wamefanikiwa kulitoa kwa sababu vifaa/vitendea kazi wao wanavyo vya kutosha vya aina yote. Na vile vile hata huko uraiani kuna makampuni makubwa yanavuo ila ni gharama kuvikodi asiniaminishe eti bila jeshi ni kuwa hilo gari eti ndo lisinge kaa litolewe.
 
Wee unataka kunipeleka niamini kuwa hilo gari bila jeshi lisingekaa litolewe hapo kabisa. Ni kitu ambacho mimi bado ni ngumu kiniaminisha bado
Tuliza akili basi kaka, mbona unaonekana ni mtu mapepe sana?. Hiyo Gari ni Mali ya mtu binafsi, na kwasababu ndani hakuna mwili wa kuopolewa, hakuna ulazima wowote wa Serikali kuingilia kati, alipaswa kufanya juhudi zake binafsi kulitoa, au aliache hapo Kama wanavyoacha watu wengine.

Alitumia makampuni binafsi kuifanya hiyo kazi kwa takriban siku kumi, lakini yameshindwa huku yakitoa sababu mbalimbali, ikiwemo kina cha MAJI, kasi ya MAJI, uzito wa Gari na mzigo uliobeba, kukosekana kwa wazamiaji mahiri.

Sasa wewe unasema ninstaka kukuaminisha nini wakati hao waopoaji wenyewe wa kibinafsi wamesalimu amri?. Huyu mama mwenyewe hili Lori amesema kama kuna mtu, kampuni au shirika lolote lenye uwezo wa kulitoa wanaomba wajitokeze, mbona hakuna hata mtu mmoja aliyejitokeza?

 
Jeshi wametoa kwa kulisukuma?

Yaani sijui nikutukane mtusi mkubwa wa kwenye chupi yako ndio unielewe au?

Nimesema hivii!!!jeshi wao wamefanikiwa kulitoa kwa sababu vifaa/vitendea kazi wao wanavyo vya kutosha vya aina yote. Na vile vile hata huko uraiani kuna makampuni makubwa yanavuo ila ni gharama kuvikodi.asiniaminishe eti bila jeshi ni kuwa hilo gari eti ndo lisinge kaa litolewe.
Huyu mama amesema kama kuna kampuni lolote lenye uwezo lijitokeze, wapi anekuambia kwamba yamejitokeza lakini amedhindwa kulipa?. Wacha kuzungumza vitu toka kichwani mwako.https://youtu.be/3u5MXSmvWF0

Hivi unajua uwezo wa kufanya kazi unategemea kuwepo kwa hivyo vitendea kazi, ujuzi, watu, mtaji na isimamizi bora, kukosekana kwa hivyo vifaa ndio kushindwa kazi, sasa utasemaje hawajashindwa ila ni kwasababu hawana vifaa?
 
Back
Top Bottom