Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kauli hiyo ameitoa leo wakati akitoa mafunzo yaliyoandaliwa na mtandao huo kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuwajengea uwezo Askari wa kike Jijini humo ambapo amewataka kutambua malengo mazuri ya kuanzishwa kwa mtandao huo.
Sambamba na hilo amebainisha kuwa Jeshi hilo halitasita kuchukua hatua kwa baadhi ya Askari wa kike ambao watabainika kutenda vitendo vya utovu wa nidhamu ikiwa ni pamoja na kuiga tamaduni mbaya za mataifa mengine.
Aidha, amewataka kuhakikisha wanayatumia mafunzo hayo ili kuujua vyema mtandao huo juu ya malengo na madhumuni ya kuanzishwa kwake sambamba na kwenda kuboresha utendaji wa kazi na kutoa huduma bora kwa Wananchi.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua amesema askari wa kike wa Mkoa huo wamekuwa wakifanya kazi zote kwa kushirikiana na askari wakiume kitendo kilichopelekea Mkoa huo kuendelea kutoa huduma bora kwa wenyeji na wageni wanafika katika Mkoa huo.
Nae Mwenyekiti wa mtandao huo Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Debora Lukololo amesema kuwa watahakikisha wanayatumia mafunzo hayo vyema ili kuleta ufanisi wa utendaji wa majukumu ya askari wa kike Mkoa wa Arusha.