Baada ya mapumziko ya siku 2, hatimae TPL inaendelea leo (24/10/2018) tena. Bingwa Mtetezi, Simba SC anawakaribisha 'Watoto wa Sekondari' Alliance FC katika dimba la Taifa Stadium. Mechi hii inatarajiwa kuanza mnamo saa 1 (moja) kamili usiku.
Katika mechi zao za mwisho Simba SC alitakata vilivyo kwa kuwagagadua ipasavyo Stand United 3-0, huku Alliance FC ikifungwa na Yanga SC. Katika mechi ya leo, Alliance FC watajaribu kutafuta pointi, huku Simba SC akitarajiwa kuendeleza wimbi lake la ushindi.
Simba SC 5-1 Alliance FC