TPL: Simba SC vs Yanga SC - Sept 30, 2018 (FT: 0-0)

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Hatimaye 30/09/2018 imefika. Leo ni siku ambayo ilikua ikisubiriwa kwa hamu sana ambapo, Bingwa Mtetezi wa TPL, Simba SC atamkaribisha Yanga SC katika dimba la Taifa Stadium.

Mechi hii inatarajiwa kuanza mnamo saa 11 kamili.

Update 1.
Jeshi La Maangamizo la Simba SC
Kikosi Cha Kwanza
1. Aishi Manila
2. Shomari Kapombe
3. Mohammed Hussein
4. Erasto Nyoni
5. Pascal Wawa
6. James Kotei
7. Jonas Mkude
8. Clatous Chama
9. Meddie Kagere
10. Emmanuel Okwi
11. Shiza Kichuya
Kikosi Cha Akiba
1. Deogratius Munishi
2. Paul Bukaba
3. Asante Kwasi
4. Said Ndemla
5. Mo Ibrahim
6. Adam Salamba

Update 2.
Kikos cha Yanga SC
1. Benno Kakolanya
2. Paul Godfrey
3. Gadiel Michael
4. Vicent Andrew 'Dante'
5. Kelvin Yondani (C)
6. Feisal Salum 'Fei toto'
7. Deus Kaseke
8. Papy Tshishimbi
9. Herietier Makambo
10. Ibrahim Ajibu
11. Mrisho Ngasa

SCORE UPDATES:

Hadi mapumziko (HT): Simba 0-0 Yanga (Kipindi cha kwanza kimetawaliwa zaidi na Simba)

SCORE UPDATES:

FT: Mpira umeisha.. Simba SC 0-0 Yanga SC

Watani wa Jadi, Wekundu wa Msimbazi Simba SC na Yanga Africans leo wametoshana nguvu ndani ya dimba la uwanja wa Taifa baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana ikiwa ni muendelezo wa michezo ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.

Simba ambayo ni mabingwa watetezi wa kombe hilo walionekana kumiliki mpira kwa muda wote wa mchezo huku washambuliaji wake wakiongozwa na Meddie Kagere wakikosa umakini katika kumalizia nafasi ambazo walizipata.

Katika mchezo huo Simba ilifanikiwa kupata kona 10 huku Yanga wakipata kona moja lakini safu nzuri ya Yanga chini ya Nahodha, Kevin Yondani iliweza kusimama imara ingawa kipa wa mabingwa hao wa Kihistoria, Benno Kakolanya anapaswa ashukuriwe kwa kuokoa idadi kubwa ya mashuti yaliyoelekezwa langoni mwake.

Huu umekua ni mchezo wa kwanza pia kwa makocha wa timu zote mbili, Patrick Aussems wa Simba raia wa Ubelgiji na Mwinyi Zahera wa Yanga ambaye ni Mkongo.

Kwa matokeo hayo, Yanga inafikisha alama 13 na kukwea hadi nafasi ya pili sawa na Mtibwa Sugar, huku Yanga ikisalia nafasi hiyo kutokana na uwiano mzuri wa magoli ya kufungwa na kufunga.

Simba inaongeza alama moja na kufikia alama 11 na kukwea hadi nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu huku Mbao Fc ya Mwanza ikiendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi kwa alama zake 14.
 
Wanaongoza kwa kufunga magoli mpaka sasa.
1. MK14 (Simba SC) - 4
2. Eliud Ambokile (Mbeya City) - 4
3. Alex Kitenge (Stand United) - 3
4. Stamili Mbonde (Mtibwa Sugar) - 3
5. Bigirimana Blaise (Stand United) - 3

Nilichogundua kwenye hii orodha ni;
Kama yule jamaa aliyewafunga Ndala goli 3 hajawahi kufunga tena.. Sasa yule MK14 ambae hashikiki katika upachikaji magoli atawafanya nini hawa Ndala?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafasi ya hizi timu katika Msimamo wa TPL
3. Yanga SC - Point 12
5. Simba SC - Point 10

Namuona mnyama mkali mwituni akienda kupindua meza kibabe siku ya leo.
 
Uimara wa safu za ulinzi mpaka sasa
1. Simba SC kafungwa vigoli viwili tu
2. Yanga SC kafungwa magoli manne

Ikumbukwe mpaka sasa Simba SC kacheza mechi nyingi ukilinganisha na Ndala.
 
Kaa kimya hujui mpira wewe.....
Unajua idadi ya magori yaliyofungwa na Yanga?. Kwa idadi ile halafu hakuna mwenye goli 3 ndo ujue yeyote kwa Yanga anakufunga hawana mfungaji mmoja na ndio timu inatakiwa iwe hivyo....ficha umbumbu wako
 
Kaa kimya hujui mpira wewe.....
Unajua idadi ya magori yaliyofungwa na Yanga?. Kwa idadi ile halafu hakuna mwenye goli 3 ndo ujue yeyote kwa Yanga anakufunga hawana mfungaji mmoja na ndio timu inatakiwa iwe hivyo....ficha umbumbu wako
Kumbuka mpaka sasa Mnyama mkali kafungwa vigoli 2 tu, pamoja na kucheza mechi kibaoooo.. Moja kati ya hayo magoli tulifungwa na Mbao kwa nguvu ya sayansi ya kiafrika.
Kwa ile beki yenu iliyooza lazima MK14 awageuze geuze anavyotaka.. Hapo bado kuna CR7 toka Uganda.. Kuna Kichuya.. Kuna Mo.. Kuna Super Sub Salamba.. n.k
Kwa kifupi leo pona yenu msiingize timu uwanjani.. Kama mnabisha, ingizeni timu uwanjani muone.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona mmekutana mambumbumbu mnajazana ujinga tu. Time is the best answer, subirini hiyo sa 11. Kambi Morogoro kazi uwanjani hatuna mbwembwe za uturuki wala kufuga mabeberu sisi.

Tambwe akiwakosa leo Ajib hawaachi. Usimsahau Makambo
Hahaha.. Leo ndo tunaionesha dunia rasmi kile tulichokifata Uturuki.
Alafu huyo Ajibu, au Mama Kambo tushawaandalia ulinzi wao.. Karibuni Taifa mshuhudie Kiama Chenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha.. Leo ndo tunaionesha dunia rasmi kile tulichokifata Uturuki.
Alafu huyo Ajibu, au Mama Mambo tushawaandalia ulinzi wao.. Karibuni Taifa mshubudie Kiama Chenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Chonde chonde kama mmeshaenda kwa waganga msithubutu kuleta timu uwanjani. Pia msije na matokeo yenu uwanjani inatosha kuzidi kulitia taifa hasara kwa furastresheni zenu. Matokeo yatapatikana baada ya dkk 90.
 
Chonde chonde kama mmeshaenda kwa waganga msithubutu kuleta timu uwanjani. Pia msije na matokeo yenu uwanjani inatosha kuzidi kulitia taifa hasara kwa furastresheni zenu. Matokeo yatapatikana baada ya dkk 90.
Hahaha.. Mkuu hii mechi tushaimaliza. Tunasubiri saa 11 tukamilishe ratiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…