TRA: Ambao hawajaitwa kwenye Usaili wa mchujo na wanadhani wana sifa, waasilishe malalamiko

TRA: Ambao hawajaitwa kwenye Usaili wa mchujo na wanadhani wana sifa, waasilishe malalamiko

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,566
Reaction score
4,013
Kufuatia tangazo la kuitwa kwenye usaili wa Mchujo wa kuandika lililotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) tarehe 22.03.2025. Katika kuhakikisha kuwa kila mwombaji anapata haki anayostahili, Mamlaka inapenda kuwafahamisha waombaji ambao hawajaitwa kwenye usaili wa mchujo na wanadhani wana sifa kulingana na nafasi walizoziomba lakini hawakuitwa, wawasilishe barua zao za malalamiko kwa Kamishna Mkuu, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndani ya siku mbili kuanzia tarehe 24 hadi 25 Machi 2025, wakieleza sababu za kudhani wanastahili kuitwa kwenye usaili wa mchujo na kuainisha nafasi walizoomba, na sifa walizonazo.

Barua hizo ziambatishwe na nakala ya barua aliyoombea kazi awali na vyeti husika.

Fursa hii imetolewa kwa waombaji waliowasilisha maombi yao toka awali. Barua zitumwe kupitia barua pepe [email protected] au [email protected].

Kwa waombaji waliopo Mkoa wa Dar es Salaam wanaweza pia kupeleka barua hizo kwenye ofisi ya TRA ya kituo cha Huduma kwa Mlipa Kodi kilichopo Mtaa wa Samora jengo la vioo la NHC HOUSE jirani na makao makuu ya TTCL wakati wa saa za kazi.

IMG_4073.jpeg
 
Back
Top Bottom